HOTELI ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro imeandaa tamasha la bia la siku 3 maarufu kama ‘Oktoberfest’ ambalo linatarajiwa kufanyika kwa mara kwanza Tanzania kuanzia Oktoba 6 hadi Oktoba 8 mwaka huu.
Akizungumza leo Septemba 6, 2023 Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Alexander Eversberg amesema nia yao ni kuona tamasha hilo lifanyika kila mwaka hotelini hapo, akisema hii ni kwa mara kwanza kufanyika Tanzania.
“Tunayofuraha kuwaletea ladha ya Tamasha kubwa kabisa la Folkfest duniani linalovutia wageni zaidi ya milioni 6 kutoka Munich, Ujerumani hadi Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha limepitishwa katika miji kote duniani.
” Lengo letu ni kushiriki utamaduni na uzoefu wa tamasha hili kwa njia halisi iwezekanavyo, kwa hivyo mgeni anaweza kutarajia bendi ya Oompha ya vipande 7 ambayo tunasafiri kwa ndege kutoka Munich Ujerumani na vile vile vyakula asili vya Kijerumani vilivyotayarishwa na timu yetu ya upishi.”
Amesisitiza tamasha litaanza Oktoba 6 hadi 8 Oktoba, hivyo wanayo furaha kuwatangaza kwamba siku ya kwanza ya hafla hiyo tayari imeuzwa na wanatarajia siku pili ya tamasha hilo zenye mafanikio zaidi.
Amewataja washirika wao katika tamasha hilo ni Achelis – Mshirika wao wa Dhahabu, Twiga Cement – Mshirika wao wa Fedha, Clouds FM – Bronze Partner na Kampuni ya Bia Tanzania TBL
“Hakuwezi kuwa na tamasha la bia bila bia, kwa hiyo tumeshirikiana na Tanzania Breweries pamoja na Crafty Dees. Mbali na bia, tutatoa divai na vinywaji vikali pamoja na Jägermeister.
“Tiketi tayari zinapatikana kwa mauzo na zinaweza kununuliwa moja kwa moja kutoka Hyatt Regency Dar es Salaam, au mgeni anaweza kutupigia simu kwa uhifadhi na malipo ya tikiti.Kiingilio cha kawaida ni Sh.40,000 pamoja na bia moja, ” amesema
Kwa upande wake Fatma Hamis ambaye ni Meneja Matukio na Uhusiano wa Wateja Wakubwa (Key Account) kutoka Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) amesema kampuni hiyo inafurahi kuunga na Hyatt ambaye ni mshirika wao na mteja wetu wa muda mrefu.
“Tunafanya naye vitu tofauti tofauti kwenye bia zetu tofauti na mambo mengine , kwa hiyo tutakuwa pamoja na Hyatt kwenye tamasha hilo, hivyo tunawaalika watu wote na tunaahidi watapata huduma bora na bidhaa bora kutoka kwa Hyatt na Kampuni ya TBL.”