Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan sl anatarajia kupokea marais Saba watakaoshiriki mkutano wa jukwaa la mifumo ya chakula Afrika AGRF lakini pia kukutana na vijana na kupokea taarifa namna vijana wa Afrika wanavyojihusisha na kilimo lakini pia kutumia fursa mbalimbali za kilimo.
Akizumgumza Septemba 6 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Marais Saba wataongozana na Rais Dkt Samia katika majadiliano ya namna Bora ya kuboresha sekta ya kilimo lakini pia kutaja fursa zilizopo nchini.
Aidha Msigwa amesema kuwa mkutano wa Jukwaa la Mfumo Jukwaa la Chakula Afrika (AGRF ) mpaka Sasa wadau mbalimbali wameanza kunufaika kwa kujadiliana fursa kwa pamoja.
Amesema wamejadiliana fursa mbalimbali zilizopo ndani na nje ya Bara la Afrika na katikamkutano huo.
“Baada ya mkutano wa vijana maraisi wote watakutana kwenye Summit watakuwa na majadiliano na watapokea taarifa mbalimbali na maadhimio ya mkutano yatasomwa kesho baada ya majadiliano, “amesema Msigwa.
Amesema Rais Dk.Samia anatarajia kuzungumza na vijana namna ambavyo anaona mwelekeo sahihi kwa Bara la Afrika kusaidia vijana kupata ajira kupitia kilimo.
Amsema wanautarajia kuwa na mairais saba wa nchi tofauti watakao hudhuria mkutano wa kesho wa AGRF ambao umehudhuriwa na watu 5000 kutoka nchi 70 za Afrika.
Gerson amesema Rais Detroit.Samia amewaalika wageni mbalimbali kwa chakula jioni na ambapo itatolewa tuzo ya mzalishaji Bora wa chakula Afrika lengo kutambua mchango wa uzalishaji chakula.
Amesema moja ya changamoto Afrika ni Upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maaneo.



