Na Sophia Kingimali
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanganyika Flavour Limited, Alpha Nondo ameishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wazawa na kuwapa fursa mbalimbali ikiwemo kushiriki katika Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) Kwani umewakutanisha na wadau wapya
Akizumgumza na waandishi wa habari Sptemba 5 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo lilipotembelea banda lililopo kwenye Ukumbi wa Mikutano Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) amesema kupitia mkutano huo wameweza kukutana na wadau na kujifunza teknolojia Mpya ambazo zitawasaidia kuboresha biashara Yao.
.Amesema lengo kubwa ni kutangaza samaki na dagaa wanaopatikana katika Ziwa Tanganyika ambao hawapatikani sehemu nyingi ili duniani itambue.
“Mkutano huu utabadilisha fikra zetu mkutano utasaidia network kila mtanzania aliyebahatika kushiriki mkutano huu atambue ni fursa ya kutangaza bidhaa na biashara yake kimataifa, ” amesema Nondo.
Amesema biashara ya samaki wanauza nchini na nchi ya Marekani wanatarajia kufungua matawi nchi nyingine na kwa mwaka huu wameingiza tani 5 za samaki nchini humo.
“Changamoto watu wa nje wanapenda samaki wa kubanikwa kutokana na changamoto hii tumebuni mashine kubwa ya kukausha samaki na dagaa kwa siku tunakausha dagaa tani kumi na samaki tani nane, ” amesema.
Kampuni ya Alpha Favour Limited imeanzishwa mwaka 2017 ofisi inapatikana mkoani Kigoma lakini Lengo kuu kutumia samaki wanaozalishwa nchini na kuuza ndani na nje ya nchi.