Waziri Angellah Kairuki Aanza Kwa Kupitia Mikakati Ya Wizara Maliasili
Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, na Naibu wake Mhe Dunstan Kitandula leo wameanza kazi katika Wizara hiyo waliyoteuliwa wiki iliyopita kwa kupitishwa katika mikakati mbalimbali ya kisekta.
Akiongoza wataalamu hao, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, na wakuu wa Idara wamewaeleza viongozi hao wapya kuwa Wizara hiyo inayochangia asilimia 21 ya Pato la Taifa na 25 ya Fedha za Kigeni ina mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato la muhimu ni uwekezaji zaidi katika uendelezaji na utangazaji wa utalii.