Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Paul Sangawe akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya uendeshaji wa programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) kilichowahusisha wakurugenzi wa taasisi zinazotekeleza programu (ITAC).Kikao kilifanyika katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Septemba, 2023.
Mratibu wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) ambaye ni Katibu wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya uendeshaji wa program hiyo Bw. Salimu Mwijaka akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Afisa Kiongozi wa Mradi wa Programu ya Kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvu (AFDP) kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Bi. Amina Ussi akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya uendeshaji wa programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) wakifuatilia hoja za mwenyekiti wa kikao (hayupo pichani) walipokutana Jijini Dar es Salaam Septemba 5, 2023.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Paul Sangawe akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya uendeshaji wa programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) walipokutana Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa MbeguTanzania (TOSCI), Patric Ngwediagi akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)