Na Catherine Kuchaka— WUSM
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ameipongeza Timu ya mpira wa Miguu ya Dodoma Jiji FC kwa kufungua duka la vifaa vya michezo na kupata mwekezaji WAZAWA NET SPORTS.
Mhe. Mwinjuma ametoa pongezi hizo leo Septemba 5, 2023 jijini hapo ambapo amewapongeza kwa kuwa na huduma ya MOBILE SHOP inayowarahisishia wateja kununua Jezi na vifaa vingine kwa urahisi.
“Tunafarijika sana kuwapata wazawa wa kuweka fedha kuboresha kiwango cha ligi yetu hata ukiangalia ubora wa jezi ni mzuri, na kwa sisi tusioweza kupiga mpira tutataka kwenda nazo kwenye concert” amesema Mhe. Mwinjuma.
Mhe. Mwinjuma amewakaribisha wadau wengine kufanya uwekezaji katika michezo ili kuunga mkono juhudi za Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katika hafla hiyo, Mhe. Mwinjuma alipokea zawadi ya jezi kwa ajili ya baadhi ya Viongozi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.