Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es salaam.
Jeshi la Polisi limeipongeza Benki ya Nmb kwa namna ambavyo inashiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu hapa nchini kwa kutoa elimu na ufadhili wa vipindi ambavyo vinahusisha maswala ya ulinzi na ulinzi shirikishi katika Jamii.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. Lazaro Mambosasa wakati akipokea Jezi mbalimbali ambazo zitatumika katika Mashindano ya Polisi Jamii DPA CUP yaliyoanza September 04, 2023 ambapo amebainisha kuwa benki hiyo imekuwa mfano mzuri katika mapambano dhidi ya uhalifu hapa Nchini.
Ameongeza kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwajengea uwezo askari hao na kuwa kutanisha na Jamii na kusema kuwa mashindano hayo yanaenda sambamba na utoaji wa damu kwa ajili ya benki ya damu salama ili kusaidia Watanzania wanaopata changamoto ya damu hasa mama wajawazito wanaojifungua na majeruhi wa ajali.
Kwa upande wake Meneja mwandamizi wa wateja maalum kutoka benki ya Nmb Queen Kilnyamagoha amesema wao Nmb wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu na Jeshi la Polisi hapa Nchini huku akiweka wazi dhamira yao ya kuendelea na mashirikiano na Jeshi hilo katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Nae Afisa Michezo toka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Salum Madongo amesema tayari michezo hiyo imeanza siku ya jana huku akibainisha kuwa michezo zaidi ya kumi na sita itachezwa katika mashindano hayo ya Polisi Jamii DPA CUP.