Na Sophia Kingimali
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewataka washiriki wa mkutano wa mifumo ya chakula Afrika AGRF kujikita kwenye mjijadala ya namna nchi itakavyoweza kujilisha yenyewe na kulisha nchi nyingine kwa kuzingatia kilimo kinavyoweza kuwa biashara na si mtindo wa maisha kama ilivyozoeleka.
Hayo ameyasema leo septemba 3 jijini Dar es Salaam wakati wa Hafla ya pembeni ya jukwaa la mifumo ya chakula AGRF ambapo mkutano wake unatarajiwa kufanyika septemba 5 mpaka 8 kwenye ukumbi wa mikutano wa jlJulius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Amesema nchi inapaswa kuondokana na unyanyapaa kwa kuona kilimo kama kipengele kilichoshindwa badala yake kinaweza kuwa cha kisasa kwa kuhamasisha na kuwezesha vijana na wanawake kuingina kwenye kilimo.
“Tunapaswa kuondokana na huu unyanyapaa wa kufanya kilimo kama cha mwisho au cha watu wasio na uwezo badala yake tunaweza kuhamasisha vijana na wazee kuingia kwenye kilimo na kukifanya kuwa kilimo cha kisasa na chenye tija kwa kuwarahisishia upatikanaji wa mbegu zilizoidhinishwa”amesema Bashe.
Aidha Bashe amesema kuwa bara la Afrika linapaswa kukabiliana na umaskini kwa kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika kilimo na uzalishaji.
Mkutano uliofanyika leo septemba 3 wa Agri Busines umejadili mazao ya kilimo kama nafaka,kunde na mbegu za mafuta ikiwa ni sehemu ya mazungumzo ya mipango ya mpango wa kuhifadhi mbolea na mbegu (FSSI)