Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alizungumza katika majadiliano yaliyoandaliwa na Shirikisho la wenye viwanda Tanzania CTI kuhusu uhana wa fedha za kigeni hasa Dola ya Kimarekani lililofanyika Leo Septemba 4, 2023 kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba akifafanua jambo katika majadiliano hayo yaliyofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya akimkaribisha Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ili kuzungumza katika majadiliano hayo.
Bw. Leodgar Tenga Mkurugenzi wa CTI akitambulisha na kuwakaribisha wage is mbalimbali katika majadiliano hayo.
……………………….
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na uhaba wa Fedha za kigeni kwa kutengeneza sera za fedha ikiwemo kuuzaji wa dolla za Marekani kwa bei ya Soko.
Akizungumza na Wanachama wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) leo Septemba 4, 2023 Jijini Dar es Salaam kuhusu uhaba wa Fedha za kigeni ikiwemo Dolla za Kimarekani na hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa wanaendelea kuchukua hatua za muda mfupi, kati na mrefu ili kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki katika uchumi.
Dkt. Nchemba amesema kuwa pia wamechukua hatua ya kufanya mapitio ya uongozaji wa soko la fedha za kigeni pamoja na kupitia kanuni za maduka ya kubadilisha fedha na kuendelea kutoa leseni kwa wamiliki wanaokidhi vigezo.
“Hivi karibuni tumefungua maduka ya kubadirishia fedha za kigeni 80 kwa ajili ya kubadirishana na ili kukabiliana na uhaba wa Fedha za kigeni” amesema Dkt. Nchemba.
Ameeleza kuwa katika kipindi cha Machi hadi Agosti 2023 wastani wa Dolla milioni 62 zinatolewa kila mwezi kwenda sokoni.
Hata hivyo Dkt. Nchemba ametoa wito kwa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania CTI kuzalisha bidhaa toshelevu ili kupunguza hofu ya upatikanaji wa dolla.
“Tuzalishe bidhaa za kutosha na kupunguza kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ambazo sisi wenyewe tunaweza kuzalisha” amesema Dkt. Nchemba.
Hata hivyo amewakumbusha wadau mbalimbali wa viwanda kuchangia fursa ya mfuko wa dhamana kwa wakopaji wanaozalisha bidhaa za kuuza nje ya Nchi.
“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maalekezo ya kufufua mfuko wa dhamana kwa wakopaji wanaozalisha bidhaa za ndani na kuuza nje ya Nchi naomba tujitokeze kuchangia mfuko huo ili fursa hiyo iweze kusaidia na kukuza wafanyabiashara wetu ” Dkt. Nchemba