Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu mapema leo akikabidhiwa ofisi na vitendea kazi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
Mhandisi Kemikimba katika hafla hiyo fupi amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini katika kipindi chote ambacho ameitumikia ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Pamoja na hayo amemtakia majukumu mema Katibu Mkuu anayechukua nafasi yake kuwataka watumishi waSsekta ya Maji kumuunga mkono kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kuchapa kazi kwani Tanzania inamhitaji kila mmoja kwa nafasi na majukumu yake.
Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maji wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Katibu Mkuu. Kutoka kushoto walioshika maua ni Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri, Katibu Mkuu Profesa Jamal Adam Katundu na aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiagwa ofisini kwake na aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba mara baada ya kukabidhi ofisi mapema leo jijini Dar es Salaam.