Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza baada ya kufungua Kituo kipya cha Polisi Mavurunza, Wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2023. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo kipya cha Polisi Mavurunza, Wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2023. Watatu kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba na wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Murilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa cheti cha pongezi kwa kiongozi wa ulinzi shiriki kata ya Kimara, Hamidu Kimtu baada ya a ufunguzi wa Kituo kipya cha Polisi Mavurunza, Kimara Wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2023. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Murilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiwaaga wananchi wa Kimara, Wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua Kituo cha Polisi Mavurunza Wilayani humo, leo Septemba 3, 2023. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………
wanafanya shughuli zao za kiuchumi kwa amani na usalama usiku na mchana ili kukuza uchumi wa Nchi na uwekezaji kama Serikali ya awamu ya sita ilivyodhamiria.”
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba alisema katika kuhakikisha usalama unadumishwa atashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha jijini hilo linakuwa salama na wananchi wanafanya shughuli zao kwa amani.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, amemshukuru Waziri Masauni kwa kuja kufungua kituo hicho, na pia amewapongeza wananchi wa eneo la Mavurunza katika jimbo lake kwa kujitoa katika ujenzi wa kituo hicho ambacho kilidumu kwa muda wa mrefu.
“Najua Askari wetu hawana chama na hawatatoa huduma kwa upendeleo ila kituo hiki kimejengwa kwa nguvu kubwa na Chama cha Mapinduzi kupitia uongozi wa Kata, Mhe. Waziri tuna ahadi kubwa tano ambazo tuliahidi kwa wananchi wa hapa Kimara ikiwemo ujenzi wa kituo hiki, barabara ya Kikwete Highway ambayo ina urefu wa Kilomita Saba, na inatarajiwa kukamilika kabla ya mwaka 2025.
Barabara hiyo itatua Bilioni 17na tayari imeidhinishwa kwa ujenzi pamoja na Hospitali ya Wilaya itajengwa eneo la Baruti, tutakamilisha miradi hii kabla ya Mwaka 2025 ili wananchi wapate huduma bora,” Alisema Prof. Kitila.
Pia ameongeza kuwa, Rais Samia ameidhinisha Wilaya za Ubungo na Kigamboni kuingia katika miradi ya DMDP ya ujenzi wa barabara ambapo Jimbo la Ubungo limepata Kilomita 55 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 88.5.