Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe akizungumza na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa Chakula unatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 -8 Septemba 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika Amath Pathe Sene akizungumza na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa Chakula unatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 -8 Septemba 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Andallah Ulega akizungumza na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa Chakula unatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 -8 Septemba 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Balozi William Shelukindo akizungumza na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023) Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa Chakula unatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 -8 Septemba 2023.
Na Sophia Kingimali
Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe ametoa rai kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kufuatilia bei ya mazao katika mitandao mbalimbali ya kimataifa ili kuepukana na uzushi unaoweza kujitokeza kwenye baadhi ya bei za mazao.
Hayo ameyasema Leo September 3 wakati akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus jijini Dar es salaam wenye lengo la kujadili kuhusu mkutano mkubwa wa mifumo ya chakula Afrika AGRF unaotarajiwa kufanyika September 5 mpaka 8.
Bashe amesema watanzania wengi walikua wakiaminishwa kuhusu kilimo cha Vanilla kwamba kilo Moja ya Vanilla inaweza kuuzwa kwa shilingi million 1 Hadi 1.5 jambo ambalo si kweli.
“Watanzania wanapaswa kupuuza taarifa hizo ambazo zimekuwa zikitangazwa katika mitandao mbalimbali sio kweli hiyo bei haipo hata kama ni kweli nchi ilikua na uhitaji wa zao hilo”amesema Bashe
Aidha Bashe amesema kuwa serikali hivi karibuni itatoa muongozo kuhusu zao hilo ambapo kwa sasa linaklmwa katika mikoa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kagera na Kilimanjaro.
Amesema ni kweli Tanzania ilikua na uhitaji wa zao hili hii ni kutokana na nchi ambazo zinaongoza kwa kulima zao hilo kukumbwa na majanga mbalimbali,
“Ni kweli tulikua na uhitaji wa zao hilo kutokana na nchi kama Madagascar ambao ndio wakulima wakuu wa zao hilo ilikumbwa na kimbunga lakini si chanzo cha kufikia bei ya milion 1 kwa kilo huo ni udanganyifu watanzania waupuuze wasubiri serikali itatoa muongozo kuhusu zao hilo”amesema. Bashe.