Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya Mkutano wa SEACJF, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Ignas Kitusi akizungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kuhusu Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 23 hadi 28 mwaka huu Jijini Arusha. wakati alipokutana nao kwenye Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Septemba 1,2023.
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya Mkutano wa SEACJF, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Ignas Kitusi akizungumza na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF kuhusu Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF) kulia ni Mwanabaraka Mnyukwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kituo Jumuishi Temeke kinachoshughulikia masuala ya Ndoa na Mirathi.
Essaba Machumu Mkurugenzi Msaidizi Kurugenzi ya Tehama Mahakama ya Tanzania akielezea jambo kuhusu Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 23 hadi 28 mwaka huu Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Bw. Deodatus Balile akitoa shyukurani zake kwa Mahakama ya Tanzania kuwa kukutana katika kikao kazi hicho.
……………………………
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassan anatarajia kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 23 hadi 28 mwaka huu Jijini Arusha.
Akizumgumza na Wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF leo tarehe 1/9/2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya Mkutano wa SEACJF, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Ignas Kitusi, amesema kuwa katika Mkutano huo Majaji Wakuu 16 kutoka
Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika watashiriki na kujadili mada mbalimbali ikiwemo namna gani watatumia teknolojia katika kuondoa vikwanzo katika biashara na utoaji haki.
Mhe. Jaji Kitusi amesema kuwa nchi 16 zitashiriki katika Mkutano huo zikiwemo Afrika Kusini, Angola, Boswana, Kenya, Rwanda, Lesotho, Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji, Namibia, Zanzibar pamoja na Zimbabwe.
Amesema kuwa Jukwaa hilo ni muhimu katika kukuza ushirikiano, kubadilishana maarifa na maendeleo ya mifumo ya Mahakama ndani ya eneo la Kusini mwa Afrika.
“Washiriki watapata fursa ya kujadili changamoto zinazowakabili katika mifumo ya Mahakama na utoaji haki na kukabiliana mbinu bora” amesema Mhe. Jaji Kitusi.
Amefafanua kuwa watajadili namna gani wataweza kutumia teknolojia pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji haki katika migogoro katika eneo la soko huria la biashara Barani Afrika.
“Pia kutakuwa na maonesho ya wadau mbalimbali wa Mahakama yatakayokuwa yanaendelea katika viwanja vya Hotel ya Mount Meru jijini Arusha kuanzia Oktoba 23, wadau watakaoshiriki ni Wizara ya Fedha, Biasahara, Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), TANAPA, NGORONGORO, TTB, LATRA” amesema.
Mhe. Jaji Kitusi.
Mhe. Jaji Kitusi amewataka watanzania kuchangamkia fursa za uchumi na biashara zitakazojitokeza kutokana na uwepo wa wageni ambapo pia wanatarajia kutembelea mbuga za wanyama.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF), Deodatus Balile, ameupongeza uongozi wa Mahakama kwa kuboresha utendaji wa kazi, huku akiahidi kwa niaba ya waandishi wa habari nchini Tanzania kuendelea kutoa ushirikiano katika Mkutano wa SEACJF.
Kauli mbiu katika Mkutano huo ni : Wajibu wa Mahakama za Kitaifa katika utatuzi wa migogoro kwenye eneo huru la biashara la Afrika, Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa ili kuongeza ufanisi katika utoaji haki.
Picha mbalinbali zikionesha Wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF wakiwa katika kikao hicho.