Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo, Bw. Juma Shabani akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31, 2023 kuhusu Mashindano ya Badoboda Mbungi Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31, 2023 kuhusu Mashindano ya Badoboda Mbungi Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mnadhimu Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Pili Misungwi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mashindano ya Badoboda Mbungi Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kamati ya Mashindano Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Kanuti Daudi, akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31, 2023 kuhusu Mashindano ya Badoboda Mbungi Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Usafirishaji usafiri wa bodaboda pamoja na Bajaji wakiwa katika hafla ya Uzinduzi Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayojulikana kwa jina la Bodaboda Mbungi Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni katika Viwanja mbalimbali Jiji la Dar es Salaam.
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (CMPD) leo Agosti 31, 2023 wamezindua Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayojulikana kwa jina la Tigopesa Bodaboda Mbungi Cup yanayotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni katika Viwanja mbalimbali Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumzia katika hafla ya Uzinduzi wa Mashindano ya Tigopesa Bodaboda Mbungi Cup Jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo, Bw. Juma Shabani, amesema kuwa viongozi wapo kwa ajili ya kuunga juhudi za vijana wakiwemo mafisa usafirishaji ambao wakituma Bodaboda pamoja na Bajaji.
Bw. Shabani amesema kuwa ofisi ya Mbunge imekuwa ikisaidia jitihadi za vijana katika kuhakikisha wanafikia malengo tarajiwa ikiwemo michezo mbalimbali.
“Ni wajibu wa viongozi kuwaunga mkono vijana, hatua waliyofikia ni kubwa na yenye kuleta tija kwa Taifa, pia Nimawaelekeza wawe wasafi katika kazi yao ili waweze kupata wateja wengi katika utendaji” amesema Bw. Shabani.
Katibu wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Daud Laurian amesema kuwa sekta ya bodaboda ina fursa nyingi za kiuchumi, hivyo ni muhimu kuwaunganisha na kuwaonyesha jinsi ya kuchangamkia na kunufaika na fursa hizi.
Amesema kuwa Tasnia ya bodaboda inamchango muhimu sana hapa nchini, madereva wengi wa bodaboda ni watu wenye bidii wanaolenga kubadilisha maisha yao.
“Tasnia yetu ina fursa nyingi za kiuchumi, hivyo bodaboda hawezi kukosa rasilimali za kuboresha maisha yake.” amesema Bw. Laurian.
Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha, amesema kuwa kama tigopesa wameamua kuungana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha malengo husika yanafikiwa.
Amesema kuwa wakati umefika kwa bodaboda kuishi kidijitali kupitia huduma ya Lipa kwa simu jambo ambalo litasaidia kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa kidijitali.
Pesha amesema kuwa katika mashindano hayo Tigo watatoa mafunzo ya ujasiriamali kwa maafisa usafirishaji ambayo yatawawezesha kupokea pesa kupitia Lipa kwa simu pamoja na kupata huduma mbalimbali za Tigopesa.
Afisa Mnadhimu Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Pili Misungwi, ametoa pongezi kwa uwepo wa mashindano hayo ambao washiriki ni wadau wao ambao wanatoa huduma ya usafirishaji.
Amesema kuwa ni fursa nzuri kwao kutoa elimu ili waweze kutii sheria na kubadilisha mitazamo na maono yao.
“Wakibadilika kifikra wataweza kutii sheria bila kulazishwa, ni jukwaa la kutoa elimu ili waweze kuzingatia kanuni na taratibu na sheria zote zinazotuongoza matumizi sahihi ya barabara” amesema .
Mratibu wa Kamati ya Mashindano Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Kanuti Daudi, amesema kuwa uwepo wa mashindano ni faraja kwao katika kuhakikisha wanaendelea kusimamia mpira wa miguu katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Amefafanua kuwa mashindano hayo watacheza katika Viwanja mbalimbali ikiwemo uwanja wa Uhuru, Ukombozi pamoja na Airwing, huku akibainisha kuwa timu nyingi zimeonesha nia ya kushiriki.
“Timu zinaendelea kujisajili kushiriki mashindano baada ya ratiba kukamilika tutaitoa rasmi”
Mashindano ya Tigo Pesa Bodaboda Cup 2023 yatahusisha jumla ya timu 64 kutoka wilaya 5 za Mkoa wa Dar es Salaam na semina mbalimbali zitatolewa maeneo ambayo mashindano haya yatafanyikia.
Madereva wa bodaboda watapata fursa ya kujifunza faida za kutumia Lipa Kwa Simu kama njia ya kupokea malipo.
Jumla ya viwanja vinne vya mpira wa miguu vitatumika kwa mashindano hayo, ikiwa ni pamoja na uwanja wa Machava Kigamboni, Uhuru wa Temeke, Ukombozi wa Ubungo na Airwing wa Ilala.
CMPD ni chama kinachosimamia madereva na wamiliki wa pikipiki katika Mkoa wa Dar es Salaam, kilianzishwa mwaka 2016, kinasaidia madereva wa bodaboda kupata mikopo ya pikipiki, viwanja, simu, leseni za udereva pamoja na bima ya afya kupitia taasisi za kifedha nchini.