Jumla ya Vijana 763 wahitimu wa awamu ya kwanza ya mafunzo ya programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Build a Better Tomorrow – BBT), jana ambapo walitembelea eneo la mashamba ya pamoja ‘Block Farm’ lililopo Mlazo, Ndogowe mkoani Dodoma ambapo watapatiwa na Serikali mashamba na maeneo ya makazi.
Eneo hilo ambalo lipo kwenye hatua ya maandalizi ni moja ya maeneo ambayo Wahitimu hao watakabidhiwa ardhi na hati kila mmoja kwa muda wa miaka 66.
Mratibu wa programu ya BBT, Bi. Vumilia Zikankuba amebainisha kuwa katika eneo hilo la Ndogowe zimepatikana hekari takribani 11,453 ambazo hazijawahi kutumika katika shughul za kilimo.
Aidha, Mhe. Haruni Lucas Diwani wa Kata ya Mhambako, Mlazo ameipongeza Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo wa BBT na ameahidi kutoa ushirikiano unaotakiwa katika utekelezaji wake.