Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimfariji Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kufuatia kifo cha Dada yake Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga mara baada ya kuwasili msibani katika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora leo tarehe 30 Agosti 2023.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Dada wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga mara baada ya kuwasili msibani katika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora leo tarehe 30 Agosti 2023.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga ambaye ni dada wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati wa Ibada ya kuaga mwili huo iliofanyika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Dada wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga mara baada ya kuwasili msibani katika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora leo tarehe 30 Agosti 2023.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha Dada wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga mara baada ya kuwasili msibani katika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora leo tarehe 30 Agosti 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga ambaye ni Dada wa Makamu wa Rais wakati wa mazishi yaliofanyika katika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora leo tarehe 30 Agosti 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga ambaye ni Dada wa Makamu wa Rais wakati wa mazishi yaliofanyika katika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora leo tarehe 30 Agosti 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa neno la shukrani kwa niaba ya familia mara baada ya mazishi ya Dada yake Marehemu Bi. Maria Isdor Nzabhayanga yaliofanyika katika Kijiji cha Kipalapala mkoani Tabora leo tarehe 30 Agosti 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewashukuru watanzania na waombolezaji wote walioungana na familia katika maombolezo na mazishi ya dada yake Bi. Maria Isdor Nzabhayanga.
Makamu wa Rais ametoa shukrani hizo mara baada ya mazishi ya Bi. Maria Isdor Nzabhayanga yaliofanyika katika Kijiji cha kipalapala mkoani Tabora. Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali nzima kwa maneno ya faraja na upendo wakati wote wa msiba huo sambamba na kuwashukuru viongozi wa dini, watoa huduma za afya na majirani wa Bi Maria kwa mchango wao waliotoa wakati wa uhai wake.
Awali akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema wanatoa pole na kuungana na familia pamoja na wote waliokuwa karibu na Bi Maria wakati wa Maisha yake duniani katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Waziri Mkuu amesema inapaswa kuenzi mazuri aliofanya na kuyaacha wakati wa uhai wake pamoja na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili aweze kupumzika kwa amani.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge, viongozi wa dini, vyama vya siasa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.