Na Sophia Kingimali
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli ametoa rai kwa wakulima kuweka akiba ya mazao ya chakula kwa ajili ya kukidhi familia pamoja na serikali kufungua uwanja Mpana Kwa Wakulima kufanya kilimo biashara Kwa kuuza mazoa Yao nje ya mipaka ya nchi
Akizungumza kwenye mdahalo ulioandaliwa na taasisi za Fedha na Kampuni ya habari ya Media Brain (MB) wenye lengo la kujadili fursa na changamoto zitokanazo na mkutano wa AGRF amesema wizara imeamua kufanya kilimo kuwa biashara ili kumsaidia mkulima kuweza kuwa huru katika biashara zake na kujikwamua kiuchumi.
“Tumefanya kilimo kuwa biashara Kwa kufungua mipaka ili Kila mfanyabiashara awe huru kuuza mazoa yake lakini kabla ujauza hakikisha umeweka chakula Cha kutosha Kwa ajili ya kumudu familia “amesema Mweli
Akizungumzia mpango wa Jenga kesho iliyobora(BBT )amesema uwepo wa BBT ni kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira Kwa vijana ambapo serikali imeanza kutumia vijana na wanawake kwenye mpango huo.
Amesema katika mpango wa BBT vijana na wanawake wanapatia ardhi Kwa ajili ya kulima mbegu na kuwatafutia masoko.
“Tumefanya tathimini ya kutosha ili kupunguza changamoto ya ajira na vijana na wengi kutojihusisha na kilimo ndipo tulipojua changamoto na serikali kuanza kulifanyia kazi ndipo ilipokuja swala la BBT kilimo”amesema Mweli
Ameongeza kuwa changamoto walizokuwa nazo vijana ndio imekua fursa kwenye mpango wa BBT-KILIMO kwa kutoa mitaji Kwa vijana,masoko na kuboresha Teknolojia .
Aidha Mweli ameongeza kuwa wakulima wadogo ndio kichocheo Cha uweo wa chakula Cha kutosha nchini.
Amesema katika mpango wa BBT haujaacha wakulima wadogo ambao tayar walishaingia kwenye kilimo wanaendelea kuwajengea uwezo na kuboresha miundombinu ili kuweza kulima kitaalam na kuweza kulima kibiashara.
Akizungumzia fusa zitakazopatikana kutokana na mkutano wa AGRF Kwa Wakulima wadogo amesema mkutano huo utakutanisha wadau mbalimbali wa kilimo hivyo wataweza kuongeza thamani ya mazoa Yao lakini pia kujitangaza kimataifa na kupata masoko ya nje
Amesema utayari wa nchi kulisha Dunia unachochewa zàidi na wakulima wadogo ambapo serikali inaendelea kuwaboreshea miundombinu ikiwemo kuendelea kuwajengea mabwawa makubwa ya maji Kwa ajili ya kufanya kilimo Cha umwagiliaji lakini pia kutoa mbolea za ruzuku kwa kila zao.
Akizungumzia mkutano wa AGRF amesema uwepo wa mkutano huo nchini umechagizwa na sababu mbalimbali ikiwemo utayari wa nchi kulisha Dunia lakini pia kupanda Kwa bajeti ya wizara ya kilimo kutoka Bilioni 298 mpaka bilion 979 Kwani imepelekea ufanisi mkubwa katika sekta ya kilimo.
Kwa upande wao wadau wa Fedha wakiwemo CRDB,NMB,NBC na EQUITY BANK wamesema kuwa wataendelea kusapoti wakulima ili kuboresha setka ya kilimo ili nchi kuendelea kuwa na chakula Cha kutosha na kufikia lengo la kulisha Dunia.
Mkutano mkubwa wa mifumo ya chakula Afrika AGRF unatarajiwa kufanyika mwezi September 5 mpaka 8 kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es salaam huku washiriki zaidi ya 4000 kutoka nje na washiriki wa ndani Zaid ya 500 wanatarajia kushiriki kwenye mkutano huo ambao utatoa fursa nyingi Kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo lakini pia Kwa nchi.