Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani Bw. Patrick Kipalu jijini Dodoma tarehe 29 Oktoba 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasilimali kutoka Marekani Patrick Kipalu (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi Imaculata Senje jijini Dodoma tarehe 29 OKtoba 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani Patrick Kipalu jijini Dodoma tarehe 29 Oktoba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
………
Na Munir Shemweta, WANMM
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo yavMakazi Mhe. Dkt Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani Bw. Patrick Kipalu.
Dkt Mabula amekutana na mkurugenzi huyo anayeshughulika na Programu za Haki na jitihada za Rasilimali Ardhi katika Bara la Afrika katika ofisi ya Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 29 Agosti 2023.
Mazungumzo ya viongozi hao mbali na mambo mengine yamelenga maandalizi ya Kongamano la Nne la Kimataifa litakalofanyika jijini Arusha kuanzia 12- 15 Sept 2023 likiwa na agenda kuu ya upatikanaji wa hatimilki za ardhi.
Taasisi hiyo ya Marekani ndiyo wadhamaini wa kongamano hilo linalojadili masuala mbalimbali yahusuyo masuala ya ardhi ikiwemo hati milki za ardhi