Vijana wa kikundi cha VICOBA cha Mkombozi katika halmashauri ya Mpimbwe wamefanikiwa kuongeza mtaji wao kutoka shilingi 125,000 hadi kufikia shilingi 19,500,500 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Machi 17, 2018 kikundi hichokiliposajiliwa rasmi.
Kikundi hicho kina wanachama 25 ambapo wanaume ni 17 na wanawake 8 ambao walikubaliana kuweka fedha na kukopeshana kwa ajili ya miradi midogo midogo.
Kwa sasa kikundi hicho kimekuwa mfano kwa vikundi vingine vinavyoanzishwa kijijini hapo kutokana na umahiri wake wa kubuni miradi na kuheshimu matumizi ya fedha zao.
Kikundi cha Mkombozi kinamiliki duka la shajala lenye mashine ya kudurufu makaratasi na kusafisha picha na duka la kubadilishia fedha na pia wameanzisha ujenzi wa jengo la biashara lenye vyumba vitano (fremu za biashara) ambalo limefikia hatua ya lenta na kugharimu kiasi cha shilingi 8,500,000/-.
Aidha vijana hao pia wamefanikiwa kuanzisha mradi wa utunzaji wa mazingira kwa kufuga nyuki na wana mizinga 52 ya nyuki wakubwa.
Mafanikio yao pia yametokana na ushauri wa mara kwa mara kutoka kwa viongozi wa halmashauri ya Mpimbwe pamoja mikopo ya asilimia kumi ya vijana ambapo mwaka 2018 walikopeshwa kiasi cha shilingi 3,000,000/- na mwaka 2023 wamekopeshwa kiasi cha shilingi 8,400,000/-.
Mbio za mwenge wa uhuru 2023 umefika katika kijiji hicho, ambapo pamoja na mambo mengine viongozi wa mbio hizo za mwenge walipata fursa ya kutembelea kikundi hicho.
Bwana Abdalla Shaib Kaim ambaye ni kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa amekipongeza kikundi hicho kwa kuwa na nidhamu ya fedha hali iliyowasababishia kupiga hatua za kimaendeleo.
Bwana Kaim aliongeza kuwa serikali imekuwa ikitenga asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kukopesha makundi ya vijana wanawake na watu wenye mahitaji maalum kwa lengo la kuwainua kiuchumi.
Aidha ameitaka jamii hususan vijana watakaoaminiwa na serikali na kupatiwa mikopo wawe wazalendo na waaminifu na kurejesha mikopo hiyo.
Awali mkuu wa wilaya ya Mlele Alhaj Majid Mwanga inaendelea kusimamia shughuli mbalimbali na mipango ya kimaendeleo ya serikali ya awamu ya sita