Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati akivuta kitambaa kuzindua ukarabati wa Madarasa 11, Ofisi za Walimu pamoja na Maabara ya Tehama katika Skuli ya Msingi Kizimkazi Mkunguni kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua vyumba vya madarasa vilivyokarabatiwa pamoja na chumba cha Tehama katika Skuli ya Kizimkazi Mkunguni tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Madarasa ya Skuli ya Kizimkazi Mkunguni mara baada ya ukarabati tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia pamoja na Wasanii wa ngoma za asili maarufu kama Mwanandege mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar kwenye shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia pamoja na Wasanii wa ngoma ya asili ya Zanzibar (Kibati) mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na mmiliki wa Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza Bw. Hossam Elshaer kuashiria ufunguzi wa Hoteli hiyo iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hoteli iitwayo Kwanza iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wamiliki wa Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza mara baada ya kuwasili katika hoteli hiyo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mmiliki wa Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza Bw. Hossam Elshaer wakati alipokuwa akitembelea Hoteli hiyo mara baada ya kuwasili Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi, wageni mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Hoteli iitwayo Kwanza mara baada ya kuifungua Hoteli hiyo iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa mmiliki wa Hoteli ya Kitalii iitwayo Kwanza iliyopo Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.