K-VIS BLOG, MWANZA
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umetwaa tuzo ya mshindi wa pili wa Mashirika,
Wakala na Taasisi za Umma kwenye kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye
Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki jijini Mwanza (MEATF) 2023.
Maonesho
hayo ambayo yamezinduliwa rasmi Agosti 28, 2023 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud S. Kigahe katika viwanja
vya Furahisha jijini Mwanza, yameandaliwa na Chama Cha Wafanyabiashara ya
Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), tawi la Mwanza yakilenga kuwaleta pamoja
wadau wa masuala ya baishara katika ukanda wa Afrika Mashariki ili
kubadilishana uzoefu na kutambua fursa zilizopo.
Sekta
ya Viwanda na Biashara ni wadau wakubwa wa WCF kwani waajiri kutoka sekta ya
Umma na Binafsi ni wanachama wa Mfuko huo ambao jukumu lake kubwa ni kulipa
Fidia kwa mfanyakazi atakayeumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi
alizoajiriwa kwa mujibu wa mkataba.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.
Exaud S. Kigahe (kulia), akimkabidhi kombe na cheti Afisa Matekelezo (Compliance
officer) wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Alberto Nyingo, baada ya Mfuko
huo kuibuka mshindi wa pili wa Taasisi, Wakala na Taasisiz a Umma (kundi la sekta
ya hifadhi ya jamii) katika Maonesho ya18 ya Biashara ya Afrika Mashariki
yanayoendelea katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.