Na Ahmed Mahmoud
Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za kufanya utalii wa Ndani ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro kuelekea Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi wa habari Mapema Jijini Arusha Mkuu wa hifadhi ya Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Angela Nyaki Amesema kwamba zoezi Hilo limekuwa likifanyika kila mwaka ila mwaka huu wameongeza Idadi ya wananchi kupanda mlima huo.
Amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka huu ni “kuhamasisha utunzaji wa mazingira ukanda wa pwani” hivyo tutumie fursa hii kuutunza mlima huu Kwa Faida ya wageni pia kutambua barafu inaendelea kuyeyuka.
Alisema kwamba Serikali na wadau wa Utalii ni muda muafaka Sasa kujitoa kuendelea kuhakikisha maeneo ya ukanda wa pwani tunatunza mazingira Ili yasaidie mlima Kilimanjaro kuweza kuvutia barafu kuendelea kuwepo na watalii wa kimataifa kuvutika kuja nchini kupanda mlima wetu.
Kwa Upande wake Meneja uhusiano wa kampuni ya Utalii ya ZARA Tours Ibrahimu Othman Amesema kwamba wanaouzoefu mkubwa wa kuwapandisha Watanzania kuadhimisha miaka ya uhuru kama miaka iliyopita Kwa kushirikiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ Pamoja na viongozi wa Tanapa.
Amesema ndio maana Kwa nafasi kubwa wamewashirikisha Watanzania na hii ni kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa nchi yetu kama ilivyo mwaka Jana tuliweza kupanda na mabalozi Taasisi na mashirika lakini tunaongeza wigo kuwakaribisha viongozi wote kuanzia Makatibu wakuu, Wakurugenzi wa Taasisi na Watanzania Kwa ujumla.
Awali Mkurugenzi wa kampuni ya African Slenic Safari Elisimbo Natai Amesema kwamba alisema kwamba njia ya Lemosho ni Moja ya njia nzuri zinazokuonyesha mlima wote hivyo ni fursa nzuri kwa Watanzania watakaojitokeza kufanya utalii wa Ndani kufika kujionea madhari nzuri ya mlima wetu.
“Kwani njia hii unakwenda Kwa siku nane na polepole Ili uweze kuona vizuri vilele vitatu vya mlima Shira Mawenzi na Kibo na kufika pasipo kupata matatizo mengi kitropiki Kutoka usawa wa juu ya bahari”
Kampuni ya ZARA Tours inatarajiwa Kwa mwaka huu kupandishi watalii wa Ndani 600 Kwa njia za Lemosho, Machame na Marangu tofauti na Mwaka 2022 walikuwa 178 huku mwaka 2021 wakiwa 165 .