Na Sophia Kingimali
Tanzania imetajwa kuwa nchi ya tatu Afrika kwa kilimo Cha Parachichi zenye soko kubwa Duniani ambazo ni aina ya Hass na Furte Hali inayochochea sekta ya kilimo kukua na kuwa msaada mkubwa kwa uchumi wa nchi.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari mkurugenzi wa mazoa kutoka wizara ya kilimo Nyasabwa Chimagu amesema wakulima na wafanyabiashara wanapaswa kuchangamkia fursa ya zao hilo lenye masoko makubwa nje ya nchi.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jitihada kubwa kuhakikisha zao hili linapata masoko nje ya nchi hivyo wakulima wanapaswa kuzingatia kanuni za uzalishaji ili kukidhi masoko ya nje ya nchi”amesema Chimagu
Aidha ameongeza kuwa kichocheo kikubwa cha wakulima kufikia kulima viwango vya kimataifa uhakika wa soko la bidhaa hiyo hali inayochochea wazalishaji kuwa na ari ya kuzalisha kwa tija na kuzingatia kanuni za ubora.
Aidha Chimagu ameongeza kuwa mkakati wa nchi ni kuhakikisha nchi inakuwa kwenye kumi bora duniani katika uzalishaji wa zao la Parachichi lakini pia kupanua wigo wa masoko kwa zao hilo.
Kwa sasa Parachichi aina ya Hass na Furte ndio iliyokamata soko la nje kwa sababu ya hali na uzuri wa tunda lenyewe kwa kuwa na ukubwa unahitajika na ubora.
Zao la Parachichi kwa Sasa soko lake kubwa lipo Ulaya kamaUingereza,Uholanzi, Asia ni China na India pamoja na nchi ya Afrika kusini.
Sambamba na hayo Chimagu ameendelea kusisitiza wakulima kujitokeza kwenye mkutano mkubwa wa mifumo ya chakula AGRF unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC Septemba 5 mpaka 8, 2023 kwani mkutano huo utatoa fursa nyingi za kibiashara kwa wakulima hao.