Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo ya Hazina jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, akisalimiana na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey, walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Hazina jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar.
Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali Wizara ya Fedha Bw. Japhet Justine akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (wa pili) na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Hazina jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, akimsikiliza Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey wakati wa kikao cha majadiliano kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Hazina jijini Dar es Salaam.
……
Na. Josephine Majura, WF, Dar es Salaam
Serikali imewaalika wadau wa Sekta Binafsi kutoka Uingereza kuwekeza nchini ili kusaidia juhudi za Serikali kufikia malengo yake.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey.
Mhe. Chande alisema Serikali imekamilisha utiaji saini na UK Export Finance kwenye Mradi wa Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na kuendeleza barabara ya Tunguu – Makunduchi -kilomita 28, Fumba – Kisauni-Mazizini -kilomita 13.2, na mkoani – Chake Chake and Pemba Airport kwa ukubwa wa kilomita 43.5
.
Katika kikao hicho Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Chande aliwakaribisha Wawekezaji mbalimbali kutoka Uingereza kuja kuwekeza katika sekta za uzalishaji, uongezaji thamani na utalii nchini Tanzania.
“Nakukaribisha wewe na wafanyabiashara na wawekezaji wa kiingereza kuleta mitaji yenu Tanzania ” alisema Chande.
Kwa upande wake Kamishna wa Biashara wa Ukanda wa Afrika wa Serikali ya Uingereza Mhe. John Humphrey Humphrey, alisema watashirikiana na Serikali kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika na kuendekeza kuwekeza katika vipaumbele vya kibiashara vilivyopo nchini Tanzania.