Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu uhaba wa fedha za kigeni hasa Dola ya Kimarekani na mafuta.
……………………….
Na Sophia Kingimali
KUFUATIA changamoto iliyoikumba nchi ya kukosekana kwa Dola hali iliyopelekea kupanda kwa gharama ya vitu mbalimbali ikiwemo mafuta serikali imeanza mkakati wa kukabiliana na hali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Gerson Msigwa amesema serikali imeanza kukabiliana na changamoto hiyo Kwa kununua dhahabu ambapo mpaka Sasa wameshanunua kilo 400.
Amesema pamoja na hayo serikali pia imeanza kutafuta mikopo itakayoongeza Dola pamoja na kuwapatia wafanyabiashara shilingi na wao kutoa Dola.
“Tunatoa dhaman Kwa biashara zizazouzwa nje ili tuweze kupata dola yaana mabenki yanawapa wafanyabiashara Kwa kuchangia 50%”amesema Msigwa
Aidha Msigwa ameongeza kuwa bado wanaendelea na utaratibu wa BoT kuuza Dola kwa jumla kwenye mabenki ambayo inakua imeshuka bei ili mabenki yote yawe na Dola na yapunguze viwango vya kubadilishia dola kwa wananchi.
“Tunaendele kutoa leseni Kwa wanaotaka kufungua maduka ya kubadilisha Fedha.
Msigwa amesema zàidi ya leseni 80 zimetolewa kwa wafanyabiashara hivyo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kuomba leseni hiyo kwa kuzingatia masharti mapya ya leseni.
Akitoa sababu za kukosekana Dola sokoni amesema madhara yaliyosababishwa na uviko 19 kwani uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ulisimama duniani
Amesema sababu nyingine ni vita ya Urusi na Ukrain, Mabadiliko ya tabia nchi lakini pia mabadiliko ya sera za fedha za Kimarekani.
Sambamba na hayo Msigwa amewataka wananchi kuongeza juhudi katika uzalishaji wa bidhaa ili kuongeza mauzo nje ya nchi hali itakayosaidia upatikanaji wa Dola.
Akizungumzia miradi ya kimkakati Msigwa amesema serikali kwa kushirikiana na shirikaa reli TRC wanaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa SGR kwa awamu ya kwanza kutoka Dar es salaam hadi Mwanza Km.1219 na awamu ya pili kutoka Tabora hadi Kigoma Km. 506.
Amesema thamani ya mradi huo mpaka Sasa ni Trilioni 23 pesa za Kitanzania.