Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa moja ya vipaumbele cha wizara kwa mwaka wa fedha 2022/24 ni kuimarisha miundombinu ya michezo kwa kujenga Viwanja vipya viwili Jijini Dodoma na Arusha ikiwa ni muendelezo wa kujipanga kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda.
Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Agosti 26 2023 Kibaha Pwani mbele ya Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa wakati akiwasilisha taarifa ya vipaumbele vya Wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imepanga kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na kuimarisha miundombinu ya michezo katika shule maalumu 56 za Michezo pamoja na ujenzi wa vituo vya mazoezi na kupumzikia wananchi na kwa kuanzia amesema ujenzi umeanzia katika mikoa ya Dodoma na Dar es salaam.
Naibu Waziri Mhe. Mwinjuma amebahinisha Vipaumbele vingine kuwa, ni kuendelea kugawa mikopo kwa Wadau wa Utamaduni na Sanaa vingine ambapo hadi kufikia Agosti 2023 Mfuko huo umefanikiwa kutoa mikopo katika awamu mbili yenyec thamani ya shilingi Bilioni 1,077,000,000 kwa miradi 45 ya utamaduni na sanaa pamoja na kuendelea kugawa Mirabaha kwa kazi za wabunifu na Waandishi wa fasihi.