Baadhi ya wadau kutoka sekta ya umma na binafsi wakifuatilia kikao kilichojadili na kupitia Andiko la Kitaifa la Programu ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma Agosti 25, 2023.
Baadhi ya wadau kutoka sekta ya umma na binafsi wakifuatilia kikao kilichojadili na kupitia Andiko la kitaifa la Programu ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma Agosti 25, 2023.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa akizungumza na wadau wa sekta ya umma na binafsi wakati wa kikao kilichojadili na kupitia Andiko la Kitaifa la Programu ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma Agosti 25, 2023. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama akizungumza na wadau wa sekta ya umma na binafsi wakati wa kikao kilichojadili na kupitia Andiko la Kitaifa la Programu ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma Agosti 25, 2023.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama akiteta jambo na Afisa Miradi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Asili (IUCN) Bw. Doyi Mazenzele muda mfupi baada ya kufungua kikao cha wadau kilichojadili na kupitia kupitia Andiko la Kitaifa la Programu ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma Agosti 25, 2023.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya umma na binafsi mara baada ya baada ya kufungua kikao cha wadau kilichojadili na kupitia kupitia Andiko la Kitaifa la Programu ya Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma Agosti 25, 2023.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama akizungumza jambo na Mratibu Mkazi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bi. Clara Makenya muda mfupi baada ya kufungua kikao cha wadau kilichojadili na kupitia kupitia Andiko la Kitaifa la Programu ya uhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma Agosti 25, 2023.
…………………………….
Serikali imewataka watalaamu wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi kuainisha mipango, mikakati na mahitaji ya vipaumbele vya shughuli za uhimilivu wa athari za mabadiliko ya tabianchi ili kuwezesha upatikanaji wa fedha za kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
Rai hiyo imetolewa Agosti 25, 2023 na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama wakati akifungua Kikao cha Wadau kilichopitia na kuridhia andiko la kitaifa la programu ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kilichofanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar Jijini Dodoma.
Dkt. Mkama amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokumbwa na athari za mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika ambapo hali hiyo inajidhihirisha kupitia matukio ya mvua zisizotabirika, ongezeko la joto, ukame na mafuriko na kuathiri sekta ya kijamii na kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, maji, afya, nishati, misitu n.k
Akifafanua zaidi, Dkt. Mkama amesema Katika kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na mapitio ya sera, uandaaji wa kanuni, mikakati na miongozo zikiwemo Sera ya Mazingira ya Mwaka 2021, Mpango Kabambe wa Taifa wa Mazingira wa maeneo ya Kimakakati (2022-2032).
Aidha Dkt. Mkama amesema katika kuweka msisitizo katika vipaumbele hivyo, Serikali kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (GCA) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeandaa rasimu ya Programu ya Kitaifa ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la la kutafuta fedha za kuhimili athari za Mabadiliko ya Tabianchi.
Programu hiyo inatarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajiwa kufanyika tarehe 4-6 Septemba, 2023 Nairobi, Kenya ili kuwezesha kutafuta fedha za kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi amesema Dkt. Mkama.
Kwa mujibu wa Dkt. Mkama amesema rasimu ya Andiko hilo tayari imekamilika na imewasilishwa katika Warsha hiyo ili kupata maboresho zaidi na kuridhiwa na hatimaye kuwezesha kuwasilishwa katika Kilele cha Mkutano huo wa Afrika wa Mabadiliko ya Tabianchi unaotarajia kufanyika nchini Kenya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa amewashukuru wadau na wafadhili waliofanikisha maandalizi ya andiko hilo na kuongeza kuwa Tanzania itahakikisha inatumia fursa hiyo kuhakikisha inachukua hatua madhubuti katika kuhimili athari za uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Tumefanikiwa kupata fedha kutoka GCA na AfDB…Tutahakikisha kuwa tunatumia fursa hii kufunganisha sera, mikakati na vipaumbele ili kubaini mahitaji ya fedha na shughuli za uhimilivu wa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya ufadhili amesema Kemilembe.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kimataifa cha Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (GCA) Kanda ya Afrika, Dkt. Charles Nkemachena amesema Shirika hilo litaendelea kuziwezesha nchi za Afrika kupata ufadhili wa fedha za miradi ya kuhimili athari za mabadiliko kutokana na athari hiyo kuathiri mataifa ya Bara hilo.
Kikosi kazi kilichoandaa rasimu ya andiko hilo kilihusisha Timu ya Kitaifa ya Wataalam kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Bara, Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC), Wizara ya Fedha (Tanzania Bara na Zanzibar).