Na John Walter-Manyara
Askari wa Jeshi la Polisi wa Kituo cha Bonga wanatuhumiwa kupokea shilingi Elfu hamsini ili kutoa dhamana kwa mtuhumiwa anapofikishwa kituoni hapo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Bonga Idrisa Sadick Katika kikao cha majumuisho ya Ziara ya siasa Babati Mjini leo Agosti 26,2023, anasema wamechoka hivyo wanaiomba serikali iingilie kati kuondoa kadhia hiyo.
“Yaani kimekuwa ni Kituo Cha kuwanufaisha watu, ukipelekwa pale Kituo cha polisi Bonga bila shilingi Elfu hamsini hupati dhamana” alisema Sadick
Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, amekiri kupokea malalamiko hayo na kwamba atalishughulikia mapema.
Dhamana ni ruhusa ya kuwa nje ya mahabusu au gereza anayopewa mtuhumiwa au mshitakiwa wakati akisubiri shitaka lake kupelekwa au kusikilizwa mahakamani au akisubiri hatma ya rufaa yake.