Na Sophia Kingimali
Ikiwa zimebaki siku chache tu kuelekea mkutano mkubwa wa mifumo ya chakula Afrika AGRF Vijana na wanawake wameaswa kujitokeza Kwa wingi kwenye mkutano huo ili kupata fursa ya kuweza kujitangaza,kupata masoko lakini pia kujifunza kutoka kwenye mataifa mengine Afrika na Duniani Kwa ujumla..
Akizungumza kwenye kipindi Cha dakika 45 kinachorusha na ITV mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo Nyasabwa Chimagu amesema kuna fursa nyingi zitakazopatikana wakati wa mkutano na baada ya mkutano ikiwemo uwekezaji na masoko.
Amesema kufuatia mageuzi ya mifumo ya chakula serikali imetenga milioni 800 Kwa ajili ya kusaidia vijana na wanawake kijiendeleza katika kilimo.
“Serikali imetenga pesa hizo kwa ajili ya vijana kwani wao wataweza kujiajili lakini pia kutengeneza ajira kwa wenzao ambapo swala hilo tunaamini litakuza mnyororo wa thamani”amesema Chimagu
Aidha ameongeza kuwa fursa mbalimbali zitakazopatika katika mkutano huo wa AGRF pia kutakua na mikataba (MoU) mbalimbali itakayosainiwa ili kukuza na kuendeleza miradi itokanayo na kilimo.
Akizungumzia uwekezaji amesema jukwaa la AGRF uwekezaji utakaojitokeza katika mkutano huo pia utakua fursa kwa wakulima wadogo,wakati na wakubwa kupata masoko na kukuza biashara zao.
“Tukizungumzia uwekezaji ni swala pana sana kutakuwa na uwekezaji kwenye kilimo utalii,uzalishaji wa mbegu na usafirishaji ambapo matumizi makubwa ya teknolojia yanahitajika ili kuhakikisha mnyororo wa thamani unakua”amesema Chimagu
Sambamba na hayo Chimagu amesema vijana na wanawake wenye ubunifu wanapaswa kujitokeza kwa wingi ili waweze kujitangaza kimataifa.
Akizungumzia mchango na ushiriki wa wakulima wadogo amesema utoshelevu wa chakula wa asilimia 100 uliopo nchini ni mchango wa wakulima wadogo,
“Wakulima wadogo wanapaswa kuwa na mpango wa kukua na si kubaki walipo AGRF inawahusu wakulima wote wakulima wadogo watanufaika na elimu watakayopata ili kukua lakini pia kupata masoko ya mazoa yao”amesema
Kwa upande wake meneja mkuu wa TAHA Anthony Chamanga amesema uwekezaji mkubwa hasa walitumia Teknolojia unahitajika ili kukuza sekta ya kilimo nchini.
Amesema uwepo wa mkutano wa AGRF unatoa fursa ya wadau mbalimbali wa kilimo kukaa pamoja na kuangalia namna Bora ya kuboresha sekta hiyo.
“Teknolojia inahitajika sana kukuza sekta hii lakini pia ukihitaji shamba na uzalishaji wenye tija unapaswa kutumia wataalum na teknolojia inavyozidi kukua wataalam unaweza kuwapata popote unapokua”amesema Chamanga
Nao Vijana na wanawake katika programu ya Jenga kesho iliyobora (BBT-kilimo) wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwathamini vijana na kuwa sehemu ya uwekezaji katika kuchangia na kuinua uchumi wa nchi.
Aidha wamempongeza Rais pia kwa kuwezesha nchi kuwa mwenyeji wa jukwaa la kimataifa la kujadili mustakabali wa mifumo ya chakula katika bara la Afrika AGRF ambapo wameahidi kujitokeza kwa wingi.
AGRF unatoa nafasi ya kutangaza fursa za uwekezaji na biashara katika sekta ya kilimo na kuonyesha utayari wa nchi kulisha bara la Afrika na Dunia.
Mkutano wa AGRF unatarajiwa kufanyika Septemba 5 mpaka 8 jijini Dar es salaam kwenye kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) ambapo washiriki zaidi ya 3000 wanatarajia kushiriki.