Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari ,Selestine Kakele akizungumza katika Mkutano huo jijini Arusha.
Mkurugenzi wa huduma za mawasiliano kutoka wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha .
Julieth Laizer, Arusha.
Kamati nne za kiufundi zimekutana jijini Arusha katika mkutano wa 41 wa baraza la utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) ili kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na mashirika ya posta barani Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha baada kufungua Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestin Kakele amesema ngazi ya kamati za kiufundi zimekutana ili kuandaa ripoti kwa ajili ya kujadiliwa na kufanyika kwa maamuzi.
Kakele amesema mikutano hiyo ni muhimu katika uendeshaji wa sekta hiyo kwani ndipo mahali ambapo maamuzi ya msingi ya kibajeti na ya kisera yanafanyika na sekretarieti kupewa jukumu la kusimamia utekelezaji wake.
Amefafanua kuwa, pamoja na mkutano huo watahitimisha na kilele cha uzinduzi wa jengo la makao makuu ya PAPU Afrika utakaofanyika hivi karibuni ambapo mgenirasmi anatarajiwa kuwa ,Rais wa Tanzania,Mhe Samia Suluhu Hassan.
Naye Mkurugenzi wa huduma za mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema kuwa jumla ya kamati nne zimekutana ili kusaidia vikao vya baraza vitakavyoanza wiki ijayo.
Sambamba na hayo amesema kuwa mashirika ya posta yana mchango mkubwa katika matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuhakikisha yanaendelea kutoa huduma katika mazingira ya sasa.