Na Sophia Kingimali
Wizara ya Kilimo Kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake pamoja bodi wametoa salam za pongeza Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuwezesha nchi kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa sekta ya kilimo barani Afrika AGRF wenye lengo la kujadili mifumo ya chakula.
Mkutano huo utatoa fursa za majadiliano ya maswala ya ustawi wa kilimo lakini pia kuvutia uwekezaji.
Aidha matokeo makubwa yanayotegemewa kupitia mkutano huo ni pamoja na upatikanaji wa masoko kwa bidhaa zinalimwa nchini lakini pia elimu ya kilimo biashara na kubadilishana uzoefu wa kilimo.
Fursa hizo ni muhimu Kwani zitaongeza ukuaji wa kilimo kwa asilimia kumi na mauzo ya mazoa nje ya nchi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 5 Hali itakayopelekea kuzalisha ajira milioni 3
Mkutano mkuu wa mifumo ya chakula AGRF unatarajia kufanyika jijini Dar es salaam September 5 mpaka 8 kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Nyerere JNICC ambapo washiriki zaidi ya 3000 watashiriki.