Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Yassir Ameir Juma akizungumza na maafisa na wapiganaji wa Chuo cha Mafunzo wakati akihamasishaji maafisa hao kujiunga na mfuko huo ,huko Makao Makuu ya Chuo hicho Kilimani Mjini Unguja .
Afisa wa Chuo cha Mafunzo Sada Nassor akiuliza suali kwa watendaji wa mfuko wa huduma za Afya walipofika kuhamasisha maafisa wa Chuo hicho kujiunga na mfuko huo, huko Makao Makuu ya Chuo hicho Kilimani Mjini Unguja
Naibu Kamishna Chuo cha Mafunzo Hamdu Haji akiuliza swali kwa watendaji wa mfuko wa huduma za Afya walipofika kuhamasisha maafisa wa Chuo hicho kujiunga na mfuko huo huko Makao Makuu ya Chuo hicho Kilimani Mjini Unguja
Maafisa na wapiganaji wa Chuo cha Mafunzo wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya dhana ya mfuko huduma za Afya Afya yaliyotolewa na Ofisi ya mfuko huo na Kufanyika Makao makuu ya Chuo hicho Kilimani Mjini Unguja.
Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Khamis Bakari Khamis akizungumza wakati akaimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko huduma za Afya Afya Zanzibar Yassir Ameir Juma kuzungumza na maafisa na wapiganaji wa Chuo hicho juu ya dhana ya mfuko huo, huko Makao Mkuu ya Chuo hicho Kilimani Mjini Unguja.
…………….
Na Rahma Khamis Maelezo.
Maafisa na Wapiganaji wa Chuo Cha Mafunzo Zanzibar wameuomba Mfuko wa huduma za Afya (ZHSF) kuharakisha malipo katika vituo vitakasvyochaguliwa kutoa huduma ili kuondosha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Wakitoa maoni katika kiao cha kuhamasisha kujiunga na Mfuko huo katika chuo cha Mafunzo magereza wamesma kuchelewa kuwasilisha fedha katika vituo hivyo kwa wakati kutazorotesha utoaji wa huduma bora vituoni humo.
Aidha walifahamisha kuwa fedha hizo zinazotoka katika mfuko huo ndizo wanazotumia kupata mahitaji ya huduma za afya kwa wananchi ikiwemo vifaa tiba.
“ikiwa tutakaa kwa muda mrefu hatujaletewa fedha ambazo zitasaidia kununulia vifaa kama madawa na vifaa vyengine wananchi wetu watashindwa kufika katika hospitali zetu na kwenda kutafuta huduma vituo vyengine,”walifafanua maafisa hao.
Mapema Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Mfuko huo Yassir Ameir Juma amewataka wananchi kuondoa hofu kwani Mfuko huo unatarajia kuufanya kila jitihada kuhakikisha hakutakua na malalamiko katika vituo vyote juu ya utoaji wa huduma hiyo.
Amesema mfuko huo utakapoanza kutoa huduma hizo kututakua na utaratibu maalumutakaotumika kwa wagonjwa ili kupunguza gharama za matumizi katika mfuko huo.
Amefahamisha kuwa mfuko hautoishia zanzibar kama baadhi ya watu wanavyosema kwani wanaandaa mikakati madhubuti kwakushirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya wa Tanzania kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma katika maeneo yao.
Aidha amesema huduma zote za msingi zitakuwepo katika mfuko huo ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa ambao wanahitaji matibabu.
Akifafanua zaidi Kaimu amesema matibabu ni msingi wa maisha ya binadamu hivyo mfuko utafanya kila jitihada kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na zauhakika bila ya usumbufu.
Aidha amefahamisha kuwa mwananchi endapo ataumwa lazima anzie Kituo cha afya kilicho karibu na endapo atapata rufaa ndipo ataendelea kwenda hospitali nyengine kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Kama hatutaweka utaratibu maalumu gharama itakuwa kubwa na ili mfuko uendelee kuwepo lazima utaratibu huo utumiwe kwani unahitaji kulindwa ili ubaki salama” alieleza.
Hata hivyo Kaimu amewataka watoa huduma kuwa na kauli nzuri kwa wagonjwa ili kuepusha malalamiko kwa baadhi ya wagonjwa .