Wakati timu ya wasichana ya Fountain Girl ikitarajia Kumenyana na Timu ya Mapinduzi Qeens ya Mkoani Njombe katika Dimba la Sabasaba ,mchezo utakaofuatiwa na michezo mingine miwili ukiwemo utakaokutanisha ma-chief Kutoka Mikoa Tofauti ya nchini na Ule wa Mashabiki wa Simba na Yanga ili kuhamasisha wananchi kushiriki katika siku tatu za maonyesho na mashindano ya ngoma,vyakula na mavazi ya kitamaduni katika Tamasha la Utamaduni kitaifa ,Serikali imetoa rai kwa mabinti kujitokeza kuonyesha vipaji wapate usaidizi.
Akizungumza katika viwanja vya sabasaba baada ya kufanyika joging ya km 5 katika viunga vya mji wa Njombe Evod Kyando ambaye ni kaimu msajili wa vyama vya michezo nchini BMT amesema kuelekea uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni ,serikali imeandaa Bonanza ambalo mechi tatu zitapigwa huku mchezo utakaokutanisha timu ya Wasichana ya Fountain Gate dhidi ya wenyeji Mapinduzi Qeeens ukivuta hisia za wengi ambapo mmsajili anasema tamasha hilo likafungue milango kwa vipaji vya mabinti kwasababu Uwanja wa Sabasaba umetoa Clara Luvanga ambaye amesajiliwa ligi ya wanawake Hispania
Kwa Upande wake Dr Resani Mnata mkurugenzi wa idara ya Utamaduni ,Wizara ya utamaduni ,Sanaa na Michezo anasema mbali na kucheza michezo hiyo lakini pia wakazi wa Njombe na maeneo Mengine wajitokeze kushiriki michezo mingine na kisha kumtaja Clara Luvanga kama shujaa wa sabasaba.
“Uwanja wa sabasaba unahistoria kubwa kwa wananjombe na mnapaswa kuuheshimu kwasababu umetoa mchezaji mkubwa hivyo na laeo njoo muone timu ya Fountain Gate iliyobeba ubingwa wa Africa watakapochea na mapinduzi Qeens,anasema Dr Resani Mnata mkurugenzi wa idara ya Utamaduni”
Katika hatua nyingine Maonyesho hayo yanatoa fursa ya kupima bure magonjwa kama vile Kisukari,Ukiwmi,ugonjwa wa moyo na mwengine mengi lengo likiwa ni kuwa na jamii salama inayojua mwenendo wa afya zao.
Wakati Mashabiki wa Simba na Yanga wakitegemea kupigakatika tamasha la kizimkazi Huko zanzibar hapa Njombe Pia Kivumbi kitaibuka.