Mkurugenzi mkazi wa AGRA Tanzania Vianey Rweyendela.
……………………..
Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea mkutano mkubwa wa mifumo ya chakula AGRF wadau wakilimo AGRA wamekutana na na wahariri wa habari nchini lengo likiwa kutengeneza uelewa wa pamoja kuhusu shughuli zinazofanywa na wakala hao.
akizungumza wakati wa mkutano huo Agost 24 jijini Dar es salaam meneja mkazi wa AGRA Tanzania Vianey Rweyendela amesema wamekuwa hawana mikakati Yao hivyo wamekuwa wakitekeleza mikakati inayowekwa na serikali katika sekta ya kilimo
Amesema AGRA imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kilimo na kuhakikisha sekta ya kilimo inakua na inakua na manufaa Kwa wananchi na Taifa Kwa ujumla.
“Kumekuwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na sekta hii ya kilimo ambayo imepelekea nchi kuwa na utoshelevu wa chakula “amesema Rweyendela
Amesema mafanikio hayo yametokana na serikali ya awamu ya sita Kwa kufanya mageuzi katika sekta hiyo Hali iliyopelekea kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa mifumo ya chakula AGRF Kwa nchi za Afrika.
“Serikali ya awamu ya sita imevunja rekodi kwenye sekta ya kilimo kumekuwa na mabadiliko makubwa sana Kwani Sasa wakulima wanalima Kwa faida”ameongeza
Amesema katika mkutano AGRF wamejipanga kuja na ripoti ya Hali ya kilimo Afrika lakini pia kuonyesha vitu vyote vizur vinavyofanywa na AGRA katika sekta ya kilimo.
Akizungumzia jitihada wanazozifanya kumkomboa mkulima amesema wameboresha kwenye ununuzi wa mbegu Kwa kuweka alama itakayomfanya mnunuzi kutambua ubora wa mbegu.
“Kila mbegu inayouzwa sokoni sasa hivi imethibitishwa Kwa kuwekewa sehemu ya kukwangua( crach) ili kujua ubora wa mbegu wapi imezalishwa na matumizi yake”amesema Rweyendela
Mkutano huo umekuja ikiwa ni siku chache zimebaki kwenda kwenye mkutano wa Afrika kuhusu mifumo ya chakula ambapo watu 3000 wanatarajia kushiriki kwenye mkutano huo utakao fanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mkutano wa mwalimu Nyerere JNICC.