Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utafiti Sera Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Suleiman Misango akizingumza na waandishi wa habari Leo kwenye mkutano uliofanyika BoT jijini Dar es Salaam kubusu upungufu wa Dolla ya Mi marekani Duniani na nchini Tanzania pia.
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kupungua kwa fedha za kigeni nchini Tanzania ikiwemo dola za marekani imechangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo vita kati Nchi ya Urusi na Ukraine, mabadiliko ya Tabia ya Nchi, mabadiliko ya sera ya fedha katika katika nchi mbalimbali ili kukabiliana na mfumo wa bei pamoja na ugonjwa wa Uviko 19.
Akizungumza leo tarehe 22/8/2023 Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na waandishi wa habari pamoja na taasisi za fedha, Mkurugenzi wa Sera na Utafiti Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Suleiman Misango, amesema kuwa
mabadiliko ya sera za nchi mbalimbali katika kukabiliana na mabadiliko ya mfumuko wa bei imechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa fedha za kigeni.
Dkt. Misango amesema kuwa katika mwenendo wa uchumi wa dunia kulikuwa na utekelezaji wa sera ya fedha kwa kupunguza ukwasi katika uchumi kwa nchi mbalimbali zilizoendelea ikiwemo Marekanii ili kukabiliana ongezeko la mfumuko wa bei.
Amesema kuwa Vita kati Urusi na Ukraine imechangia kwa kiasi kikubwa kuvurugika kwa mnyororo wa ugavi wa bidhaa na upungufu wa bidhaa katika soko la duniani.
“Nchi ya Urusi na Ukraine walikuwa hawazalishi bidhaa, hivyo mahitaji ya fedha za kigeni za kununua bidhaa yaliongezeka hasa dola za marekani” amesema Dkt. Misango.
Amefafanua kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha ukame na mafuriko na kusababisha ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni kwa nchi nyingi duniani kwa ajili kujenga pamoja kukarabati miundombinu.
“kukiwa na ukame utaitaji fedha zaidi kwa ajili ya ununuzi wa mafuta kwa ajili ya kuzalisha nishati, kununua nafaka Kwa ajili ya chakula” amesema Dkt. Misango.