RAIS wa Indonesia Mh. Joko Widodo akiwasili kwa ndege yake kwenye u wanna wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku siku mbili Tarehe 21 – 22 Agosti, 2023. ambapo amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Stergomena Tax, Balozi Makocha Tembele Balozi wa Tanzania nchini Indonesia na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila.
……………………………
Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Mheshimiwa Joko Widodo amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku mbili kuanzia tarehe 21 – 22 Agosti, 2023.
Ni majira ya saa 4:40 alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb).
Viongozi wengine walioshiriki mapokezi ya Mheshimiwa Widodo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele, Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Tri Yogo Jatmiko pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.