Na Sophia Kingimali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano maalum wa baraza la vyama vya siasa nchini utakao kutanisha wadau wa siasa lengo likiwa kuthamini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi
utakaofanyika Agosti 28 mwaka huu jijinim Dar es salaam.
Akizungumza na Fullshangwe leo Agosti 21 jijini Dar es Salaam Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi amesema mkutano huo unaotatajia kufanyika Agost 28 utawakutanisha wadau wa siasa mbalimbali ambao utafanyika Kwa siku tatu katika kituo cha Mikutano ya Kimataifa Julius Nyerere (JNICC).
Amesema kuwa lengo la mkutano huo maalum ni kujadili hali ya siasa nchini na tathimini ya utekelezaji wa ushauri wa kikosi kazi uliotolewa kwa serikali .
“Mkutano huu tunatarajia utafunguliwa na Rais Dk.Samia na unatarajia kufungwa Agosti 30 mwaka huu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ,” amesema Jaji Mutungi.