Mwenyekiti wa Wadau Group Stephen Kazimoto amewataka wanajumuiya wa umoja huo kushirikiana kwenye shida na raha bila kuwepo utengano kati yao.
Hayo ameyasema Leo Agosti 19 kwenye mkutano maalumu wa kujadili mkutano mkuu wa umoja huo unatarajiwa kufanyika disemba 9, 2023 amesema umoja huo ni mkubwa ambapo wadau wanapaswa kujisemea mema ,na mazuri popote wanapokua,
“Hii ndio Wadau Orijino tunapaswa kushirikiana tusisikilize maneno ya watu tujadili kwa pamoja kwani wadau inakua kubwa na fursa zitakukuja “amesema Kazimoto
Amesema heshima ndio msingi mkuu bila kujali elimu au uwezo wa mtu ili kukuza na kuendeleza mshikamano wao.
“Haya Maisha tunayo duniani tu hakuna mahali pengine ambapo tutaweza kukutana tukikaa vizuri tukakubaliana wadau itakuwepo vizuri na tutafika mbali”ameongeza Kazimoto
Kwa upande wake katibu wa Wadau Group Issa Mnasnha amewataka wanachama kutumia kikao hicho kujadili mambo yatakayosaidia kusonga mbele na kuimarisha umoja huo.
Mkutano mkuu wa Wadau Group unatarajiwa kufanyika mwezi ambapo utaambatana na siku maalum ya umoja huo huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwekwa wazi hivi karibuni.
Mkurano huo umepitisha Rasimu ya katiba ya Wadau Saccos ambao itasajiriwa hivi karibuni na inatarajiwa kuzinduliwa Pia Disemba 9, 2023 wakati mkutano Mkuu wa mwaka utakapofanyika.
Mkutano huo maalum pia umepitisha kwa kauli moja wanachama kuchangia shilingi elfu 50.000 kwa ajili ya kuniunga na Saccos hiyo na shilingi elfu 50.000 nyingine tena kwa ajili ya kuchangia sherehe yao itakayofanyika sambamba na mkutano Mkuu huo.