Na Sophia Kingimali
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA imetoa onyo Kwa kampuni za mabasi ya masafa marefu walioanza kufanya safari za usiku ikiwa ni kinyume Cha utaratibu.
Akizungumza Leo Agosti 18 na waandishi wa habar jijini Dar es salaam mkurugenzi wa udhibiti usafiri wa barabarani Johansen Kahatano amesema utaratibu wa magari ya masafa marefu kuanza kutembea Kwa saa 24 bado upo kwenye mchakato hivyo ni kosa Kwa mabasi kufanya safari hizo bila kufuata utaratibu.
Amesema kumekuwa na baadhi ya mabasi ambayo yameruhusiwa kuanza safari saa Tisa usiku kulingana na mahali yanapokwenda.
“Hivi karibuni kumeibuka baadhi ya makampuni yanafanya safari za usiku kinyume na taratibu tumeshapokea taarifa zao ambao tumeshwapa onyo ikiwa pamoja na kuwapiga faini”amesema Kahatano
Amesema lengo la LATRA si kutoa adhabu Bali ni kutoa elimu hivyo watumiaji wa barabara wanapaswa kusingatia elimu inayotolewa ili kujiepusha na madhara yanayoweza kutokea.
“Nitoe rai kwa mabasi ambayo yameanza kufanya safari za usiku lakini pia abiria ambao wanapanda gari hizo kuacha mara moja kwani wanahatarisha maisha yao na wakumbuke pia usiku huo Kuna baadhi ya maeneo hakuna askari wa usalama barabarani hivyo wanaweza kupata shida na wakakosa msaada”ameongeza Kahatano
Sambamba na hayo Kahatano amesema utaratibu wa mabasi kuanza kutembea kwa saa 24 upo kwenye mchakato na karibu utakamilika hivyo wamiliki wanapaswa kuanza kupeleka maombi.
Amesema maombi yao ni sehemu ya maandalizi kwani watachakata na kujua njia gani itaanza na huduma hiyo na gari zipi.
Amesema kuanza Klkwa safari hizo kunapaswa kuwa na maandalizi ikiwemo uwepo wa huduma zote muhimu njiani kama ilivyo kwenye safari za mchana ili kuondoa kero Kwa abiria watakao kua safarini Kwa nyakati za usiku.
“Safari za usiku zitaanza kwani mchakato wake unaendelea hivyo tuwaombe wamiliki kuleta maombi yao lakini pia tunahakikisha miundombinu yote inakua rafiki kwa wasafiri ikiwemo huduma za usalama”amesema Kahatano
Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilitoa agizo la kuanza safari Kwa saa 24 mwezi June wakati akiahillrisha shughuli za Bunge hivyo wizara ya uchukuzi Kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya ndani ya nchi bado ipo kwenye mchakato wa kushughulikia jambo Hilo ambapo Mamlaka ya ulUsafiri wa Ardhini LATRA watatoa ratiba ya kuanza safari hizo.