Mbunge wa Jimbo la Ilala lakini pia naibu spika wa Bunge Mussa Zungu amegawa majiko ya gesi 200 katika masoko manne yaliyopo katika wilaya ya Ilala lengo likiwa kuwasaidia kurahisisha shughuli zao lakini pia kulinda mazingira ili kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa
Akizungumza Leo Agosti 18 mara baada ya kugawa majiko hayo katika soko la machinga Complex jijini Dar es salaam amesema lengo la Rais Samia ni kumsaidia mjasiliamali mdogo kujikwamua kiuchumi huku akilinda mazingira lakini pia akiimarisha Afya yake
Amesema ugawaji wa majiko hayo utasaidia kukuza uchumi wa wananchi lakini pia lengo. La nchi la kukubiliana na changamoto ya hewa ukaa inafikia malengo
“Tunafanya haya ili kuwasaidia mama na baba lishe katika mkoa wetu ikiwa ni sehemu ya kampeni ya utunzaji wa mazingira ili tukaribiane na janga la hewa ukaa lakini pia kulinda pia kulinda Afya za wananchi wetu”ameongeza Zungu
Kwa upande wake Meneja wa Soko la machinga Complex Stella Mgumia amesema Majiko hayo yataleta tija Kwa Wafanyabiashara Kwani uchumi wao utaongezeka lakini pia watatunza mazingira
Amesema msaada huo uliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan utawasaidia wajasiliamali hao kujikomboa kiuchumi kiafya lakini pia kutunza mazingira na kupeleka kupungua Kwa magonjwa ikiwemo kifua.
“Msaada huu kiukweli umekuja muda muwafaka Kwa mama na baba lishe katika soko letu hivyo nitoe Rai Kwa ambao hawapo kwenye utaratibu rasmi wa soko kuingia kwenye utaratibu ili wasipitwe na misaada kama hii ambayo serikali inatoa Kwa wananchi wake”amesema Mgumia
Ameongeza kuwa wananchi wanazofanya biashara kando kando ya barabara lilipo soko Hilo wanapaswa kuondoka haraka Kwani ni kinyume Cha Sheria
Nao wafanyabiashara wa soko Hilo wamemshukuru rais Samia pamoja na uongozi wa soko Hilo Kwa kujali Afya zao lakini pia kuwarahisishia shughuli zao.
“Kipekee Mimi nimpongeze Rais Samia lakini mwenyekiti wetu wa soko anafanya kazi kubwa sana ya kutusaidia sisi wajasiliamali hapa amekua akutufuatilia mmoja mmoja mpaka kujua Afya zetu juzi tu walikuja madaktari hapa na wametufanyia vipimo”amesema mmoja wa baba lishe.
Mbunge Zungu amefanya ziara katika masoko manne yaliyopo kwenye wilaya ilala ambayo ni Machinga Complex,Gerezani,Ilala na Karume na kugawa majiko 200 ya gesi Kwa baba na mama lishe ikiwa ni sehemu ya serikali ya kusaidia wananchi wake kujikwamua kiuchumi lakini pia kutunza mazingira.