Naibu katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa sekta hiyo kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yatakayoweza kutatua changamoto za ardhi Mkoani Mwanza.
Kamishna wa ardhi msaidizi Mkoa wa Mwanza Happiness Mtutwa akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi.
Watumishi wa sekta ya ardhi Mkoa wa Mwanza wakiwa ukumbini.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Watumishi sekta ya Ardhi Mkoa wa Mwanza wametakiwa kutoka nje ya ofisi na kwenda kuwafata wananchi mahali walipo ili waweze kutoa huduma na kuwapa elimu juu ya umiliki wa Ardhi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika ardhi.
Hayo yamebainishwa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera katika kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa sekta hiyo Kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yatakayoweza kutatua changamoto za ardhi.
Lucy amewataka watumishi hao kuzingatia wajibu wao kama watumishi ndani ya sekta, kutekeleza wajibu kwa weledi na uadilifu pamoja na kutoa huduma nzuri kwa watanzania.
“Sekta ya ardhi ni sekta ambayo inatoa huduma kwa wananchi sasa kwa sehemu kubwa tumekuwa tukipata malalamiko kama watendaji ndani ya sekta yanayosababishwa na huduma hazilizishi ambazo zinatolewa nawatendaji wetu” Alisema Lucy.
Kwa upande wake Kamishina wa wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Mwanza Happiness Mtutwa, ameeleza kuwa wamepokea maagizo yaliyotolewa na Wizara hiyo na kuhakikisha kuwa wanatatua migogoro hiyo Kwa kuweka Kambi na kusikiliza kero za wananchi.
“Tumejipanga kwa pamoja na wenzangu wa Halmashauri zote zilizohudhulia hapa kuendelea kutatua migogoro ya ardhi Mkoa mzima” Alisema Happiness.
Baadhi ya watumishi wa sekta hiyo wameishukru Wizara kwa kutoa vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kufanya kazi Kwa weledi na kuweza kuwafikia kiurahisi wananchi hatua itakayosaidia kupunguza malalamiko yaliyopo.
“Tunaishukru sana Wizara kwa kutupatia hivi vitendea kazi kutokana na changamoto tulizokuwa nazo za upungufu wa vifaa na kutufanya tusitoke nje Kwa urahisi”