Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 17 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi.
Baadhi ya Wajumbe Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bungeni, tarehe 17 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Mendeleo ya Jamii Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akizungumza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), leo tarehe 17 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo Bi. Aziza Kheir.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akifafanua jambo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, tarehe 17 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Sophia Mwakagenda akichangia jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), leo tarehe 17 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) (waliokaa msatari wa mbele), wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, tarehe 17 Agosti, 2023, jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba.
Baadhi ya Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, tarehe 17 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa nne kutoka kulia), Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (wa nne kutoka kuhoto), Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba (wa tatu kutoka kulia) na baadhi ya watendaji wa mfuko huo mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni leo tarehe 17 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
………
Na Mwandishi Wetu: Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sekta binafsi yamechochea ukuaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Aidha, Mhe. Ndalichako amesema ukuaji huo umepelekea thamani ya mfuko kuongezeka pamoja na michango ya wanachama.
Waziri Ndalichako ameyasema hayo Agosti 17, 2023 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya NSSF kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi wa Maendeleo ya Jamii.
Amesema kwa mwaka 2022 mfuko huo uliandikisha wanachama 233,644 hadi kufikia Juni mwaka 2023 kulikuwa na wanachama 243,895 na matarajio ifikapo Juni 2024 ni kuwa na wanachama 277,279.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, ameutaka mfuko wa NSSF kuhakikisha unaongeza wanachama zaidi hasa waliopo kwenye sekta isiyo rasmi.
Akijibu hoja za wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amewahakikishia wabunge kuzingatia maoni yao ili kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama wake.