Balozi |
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe.
Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed mapema wiki hii amewasilisha Hati za
Utambulisho kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Mohammed Bin
Zayed Al Nahyan katika Ikulu ya nchi hiyo (Qasr Al Watan) iliyopo mjini Abu
Dhabi.
Viongozi hao pia walipata wasaa wa mazungumzo ambapo Mheshimiwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu alimhakikishia Mhe. Mohamed ushirikiano wa Serikali yake katika
kutekeleza majukumu yake nchini UAE kwa manufaa ya pande zote mbili hususan kiuchumi.
Kwa upande wa Balozi Mohamed alimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa atahakikisha Watanzania na Waemirati wananufaika na fursa za uchumi zilizopo pande zote mbili.