………………….
Na Sixmund Begashe
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Malikale nchini na Makumbusho ya Taifa, imerithisha historia ya Vita vya Majimaji Kwa wanafunzi na wananchi mbalimbali kupitia kongamano maalum katika Tamasha la Vita vya Majimaji Nandete Mkoani Lindi.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mhe. Farida Kikoleka amewasihi wanafunzi na Jamii kwa ujumla kuuvaa uzalendo wa Mashujaa waliopigania haki, utu na heshma ya Mtanzania na Afrika kwa ujumla kwa kusoma na kufanya kazi kwa bidii.
Sanjari na hayo, Mhe. Kikoleka ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kazi nzuri ya kurithisha kizazi kilichopo Urithi wa kipekee wa Historia ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji kwani sasa kunakasi kubwa ya mmomonyoko wa maadili hivyo elimu iliyotolewa na Maafisa wa Wizara hiyo ni Urithi sahii.
Vita vya Majimaji vilianzia Nandete Kilwa Mkoa wa Lindi Mwaka 1905 huku vikiongozwa na Jemedari Mkuu wa Jeshi jasiri la Kabila la Wamatumbi, Sikwaku Mbonde, Mkuu wa Jopo la Ufundi Mambo ya Kale na Saikolojia Bibi Nantabilwa Naukinda, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Jasiri la Wamatumbi Bw. Ngumbekumbe Mwiru na wengineo, kisha kuandelea Maeneo mengine na kuishia Mkoani Ruvuma.