Wahamiaji haramu 65 kutoka Ethiopia wakiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa kwenye geti la Kamsisi wilaya ya Mlele.
……………………………
Na Kibada Ernest – Mlele- Katavi
Agosti 14,2023
Raia 65 wa Ethiopia wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kuingia nchini kiyume na taratibu na kusafiri kwenda nje ya nchi kupitia wilaya ya Mlele bila kufuata taratibu.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Majid Mwanga akizungumzia tukio hilo leo Agosti 14 amesema kuwa wahamiaji hao wamekamatwa Kijiji cha Kamsisi kilichopo Kata ya Kamsisi kwenye kizuizi geti la maliasili majira ya saa tano mchana,ambapo Idara ya Uhamiaji ,kwa kushirikiana na Askari wa huduma za Mistu TFS na watumishi wa Halmashauri walioko kwenye geti hilo,na wale wa kwenye mizani ya Kamsisi ambao wamesaidia kukamatwa kwa lori lilolokuwa limebeba wahamiaji wahamiaji hao.
Walikuwa wanasafiri kwa gari kubwa Lori la mafuta lenye Namba za usajili T.952 DFB ambalo lilikuwa likiendeshwa na Dreva anayejulikana kwa Msadick Mohamed Msomolo Mkazi wa Mwanza,akiwa na mwenzake mkazi wa Kihonda Mkoa wa Morogoro.
Gari hilo lilikuwa likitokea Mkoa wa Mwanza kuelekea Tunduma Mkoa wa Songwe kupitia Sumbawanga Mkoa wa Rukwa,
Wahamiaji hao walibebwa ndani ya gari hilo kutoka eneo la Kisese Mkoa wa Mwanza na walikuwa wakipelekwa Tunduma Mkoa wa Songwe kwa safari ya kwenda nje ya nchi.
Kukamatwa kwa Wahamiaji hao Mkuu wa Wilaya amepongeza moyo wa uzalendo ulioneshwa na watumishi wa Idara ya Uhamiaji, Wakala wa mistu TFS,watumishi wa Wakala wa barabara upande wa Mizani na watumishi wa Halmashauri waliokuwa kwenye geti la Kamsisi waliosaidia kufanikisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza watumishi kuwa waaminifu nan a waadilifu,huku akionya wamiliki wa magari madereva kuwa waadilifu na kuacha kusafirisha wahamiaji haramu
Hakuna watu watakaokuja kutulindia nchi yetu bali ni sisi wenyewe na wajue kuwa kitu kibaya kitapita inyonga uongozi uko imara.
Wale wote wanaofikiri watapita Inyonga hawataweza kuvuka salama Wilaya ya mlele kwa kuwa hali ya ulinzi na usalama uko imara watakamatwa tu.Amesema uongozi wa Wilaya ya Mlele uko makini na hautokubali Barabara zake kutumiwa kusafirishia vitu haramu kama binadamu tena ndani ya malori ya mafuta kama mizigo na kudharirisha utu wa mtu lazima watakamatwa tu “alisema Mhe,Mwanga Mkuu wa Wilaya ya Mlele.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mhe.Soud Mbogo amepogeza kazi nzuri iliyofanikisha kukamatwa kwa wahamiaji hao na kulaani vikali hicho na kueleza kuwa hawako tayari kuona Barabara za Halmashauri ya Mlele zikitumiwa vibaya kusafirisha wahamiaji haramu.
Mhe Rais amewatengenezea barabara kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake na sikufanya mambo ambayo hayaendani na utu wa mtu kama kuwasafirisha hawa binadamu tena kwenye lori la mafuta kama mizigo kitendo hicho ni cha kinyama na wale wote waliohusika sharia ichukue mkondo wake.