Mkurugenzi wa Gazeti la Jamvi la Habari Habibu Mchange na waandishi wa habari wapatao sita wamevamiwa na kundi la Vijana wa kimasai na kujeruhiwa vibaya walipokuwa wakifanya mahojiano na wananchi wanaotaka kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.Baadhi ya waandishi wa habari waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo katika kijiji cha Endureni wilayani Ngorongoro ni Denis Msacky, Ferdinand Shayo.Akizungumza na Jambo TV ndugu Habib Mchange amemtuhumu Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Mhe. Emanuel Oleshangai kuratibu mashambulizi hayo ambapo.
Jambo TV imefanikiwa kuzungumza na Mbunge Oleshangai kuhusiana na tuhuma za kuratibu mashambulizi hayo kwa wanahabari ambapo amekanusha vikali kuhusika na uhalifu huo huku akisema hana sababu ya kuratibu mashambulizi kwa wanahabari hao . Oleshangai amesema Endureni ni kijijini kwake na aliwaona hao waandishi wa habari wakiwa mnadani wakiwakusanya watu kwa ajili ya kuzungumza nao huku yeye na viongozi wengine akiwemo Mwenyekiti wa CCM wakila nyama na baadae akaondoka kurejea nyumbani kwake.Oleshangai amesema alipofika nyumbani kwake ndio alipata taarifa ya kutokea kwa fujo hizo hivyo hahusiki nazo