Dr. Emmanuel Masenga mtafiti Mkuu TAWIRI akitoa maelezo Kwa viongozi mbalimbali akiwepo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo na kamishna mwandamizi na kamanda wa uhifadhi Kanda ya kusini mashariki TAWA Abraham Jullu namna ambavyo watatumia Helikopta kuwarudisha Tembo hifadhini
Wa kwanza kushoto ni Dr Emmanuel Masenga mtafiti Mkuu TAWIRI anayefaata ni mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo wakiwa pamoja na katibu wa mbunge wa jimbo la Nachingwea George Martin pamoja na kamishna mwandamizi na kamanda wa uhifadhi Kanda ya kusini mashariki TAWA Abraham Jullu wakati wa zoezi la kuwaondoa Tembo kwenye mazi ya watu na kuwarudisha hifadhini kwa njia ya helikopta katika wilaya ya Nachingwea mkoa Lindi
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa amepanda Helikopta Kwa ajili ya uzinduzi wa zoezi la kuwarudisha Tembo hifadhini kutoka kwenye makazi ya wananchi.
…………………………….
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
Serikali kupitia Wizara ya maliasili na utalii kwa kushirikiana na Taasisi zake ambazo ni TAWA, TAWIRI NA TFS imeendelea na kutekeleza mkakati wa kuhakikisha changamoto ya Tembo Mkoani Lindi inamalizika.
Akizungumza mara baada ya kushuka kutoka kwenye Helikopta,Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuchukua hatua za kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu huku shughuli za kiuchumi zikiendelea bila matatizo yoyote yale.
Moyo alisema kuwa Tembo wamekuwa wakiharibu mazao ya wananchi na kusababisha vifo mara kadhaa hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan akaamua kutuma timu ya wataalam kutoka TAWA, TAWIRI na TFS kushughulikia suala la kuwaondoa Tembo kwenye makazi ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Alisema kuwa Rais Dr Samia suluhu Hassan ameona imekuwa kero kubwa kwa wananchi hivyo serikali imeanzisha mpango madhubuti wa kutoa mafunzo ya kukabiliana na Tembo kwa vijana wanaotoka katika vijiji ambavyo vinasumbuliwa na Tembo.
Moyo alimazia kwa kusema kuwa ni kweli watu wawili wameuwawa na Tembo na serikali imeanza kuchua hatua za haraka kuwafukuza Tembo Kwa njia ya Helikopta.
Kwa upande wake Kamaishna Mwandamizi na ni kamanda wa uhifadhi Kanda ya kusini mashariki TAWA Abraham Jullu alisema kuwa Tembo wapo jirani na makazi ya watu hivyo jukumu lao ni kuhakikisha wanawarudisha Tembo hifadhini ili wasilete madhara kwa binadamu.
Kamanda Jullu alisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kujilinda na mnyama Tembo ili kuokoa maisha yao kabla serikali haijachua hatua za kuwaondoa Tembo hao.
Naye Dkt. Emmanuel Masenga mtafiti Mkuu TAWIRI alisema kuwa Tembo wamekuwa wanafuata maji katika mto Mbwemkuru hivyo inakuwa rahisi Tembo kuvuka mto huo na kwenda kwenye mashamba na makazi ya wananchi waliojirani na mto Mbwemkuru.
Dkt Masenga alisema kuwa wanaendelea kutafuta njia mbalimbali za kuwazuia Tembo kwenda kwenye makazi ya wananchi na kuwaomba wananchi waendelea kujilinda kutokana na elimu waliyopewa na wataalam mbalimbali wa wanyama pori.
Salma Kingwande ni mwananchi wa Kijiji cha Narung’ombe alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia suluhu Hassan kwa kupeleka chopa kuwafukuza Tembo kwenye makazi ya wananchi kwa kuwa wamekuwa wakileta maafa ya vifo na kuharibu mazao ya wananchi