Na Heri Shaaban (ILALA )
Mkuu wa WIlaya ya Ilala , Edward Mpogolo ,amezuia biashara ya midangulo Buguruni na vijana wanaohusika na biashara za madawa ya kulevya wafichuliwe.
Mkuu wa WIlaya ya Ilala Edward Mpogolo, alisema hayo Katika Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, wakati wa Mkutano wa hadhara Kata ya Buguruni .
“Natoa agizo Biashara za madanguro yote yanayofanyika Buguruni yasitishwe na vijana wanaohusika na biashara ya huuzaji madawa ya kulevya muwafichue waweze kuchukuliwa hatua “alisema Mpogolo .
Mkuu wa WIlaya Mpogolo alisema eneo la Buguruni kuna biashara ya madanguro wale watakao kamatwa watachukuliwa hatua kali amewataka wananchi kuacha kujishughulisha na biashara hizo badala yake wajishughulishe katika biashara halali ya kuwaingizia kipato cha halali .
Alisema ofisi yake ya wilaya ipo wazi wanaohusika kuendesha Biashara ya madanguro na vijana wanaohusika na uuzwaji madawa ya kulevya apelelekewe majina kwa njia ya Siri waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua .
Wakati huo huo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, amefanya maendeleo makubwa katika Wilaya ya Ilala katika sekta ya Elimu Kujenga madarasa kila ,Vituo vya afya na miundombinu ya barabara ambapo katika Wilaya ya Ilala Serikali inatarajia kujenga Barabara za kisasa za mradi wa kuboresha Miundombinu ya Jiji (DMDP )Kilometa 42 za lami .
Katika hatua nyingine mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alisema Wilaya ya Ilala sasa hivi huduma za kiserikali zimegawanywa katika Kanda tano kwa ajili ya kuwarahishisha wananchi waweze kupata huduma za kiserikali karibu na maeneo yao kuwapunguzia mzigo wa kusafiri kwenda Wilayani na Halmashauri kufuata huduma .