Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi wametembelea eneo la Hifadhi la Hifadhi ya Ngorongoro kuona vivutio mbalimbali vya utalii na kujifunza shughuli za uhifadhi.
Akiwa katika ziara hiyo Dkt. Yonazi ameeleza kuwa pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani kupitia watumishi wa Ofisi hiyo, wametumia fursa hiyo kama watunga Sera kuona uratibu wa shughuli mbalimbali za uhifadhi, utalii na kushuhudia namna juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan zilivyochangia kuongeza idadi ya wageni ambapo kwa sasa eneo la hifadhi ya Ngorongoro pekee linatembelewa na wastani wa wageni 2,500 hadi 3,500 kwa siku.