Na Sophia Kingimali
Shirika la bima la Taifa(NIC) limepokea tuzo kutoka kampuni ya Superbrand ikiwa ni matokeo ya kazi wanazofanya katika kuhudumia wananchi.
Akizungumza leo Agosti 14 mara baada ya kupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dkt. Elirehema Doriye amesema wataendelea kuja na ubunifu wa bidhaa ambazo zitagusa watu wote.
Amesema cheti hicho cha Superbrand kinaonyesha kuwa utendaji kazi wa shirika hilo na ubora wa mtoa huduma pamoja na ubora wa bidhaa na namna mteja anavyoridhika na huduma zinazotolewa.
“Leo ni siku ya kipekee kwetu kama shirika kwani ni mara ya kwanza kupokea cheti/tuzo hii ya Superbrand hii inaonyesha namna tunavyofanya kazi vizuri katika kuwahudumia wananchi kwetu huu ni mwanzo tu tutaendelea kutoa huduma Bora Kwa kila Mtanzania”amesema Doriye
Ameongeza kuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni inayomilikiwa na serikali k kupata cheti hicho haya ni mafananikio Kwa serikali na nchi.
“Hii inaonyesha ni mafanikio makubwa kwa serikali kwani hayo ni maono na maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyosababisha kufikia mafanikio haya ambayo leo ndio tunaona matokeo yake”ameongeza Doriye.
Amesema kufuatia utafiti huru uliofanywa na kampuni ya Super brand wa kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ndio umetoa mwanga wa namna bima hiyo inavyofanya kazi na kuwatofautisha na kampuni nyingine za bima.
Aidha Doriye Ameongeza kuwa wanatarajia kuboresha zàidi matumizi ya teknolojia ili kuwafikia wananchi kila sehemu..
Kwa upande wake Meneja Miradi kutoka kampuni ya Superbrand Jawad Jaffer amesema upatikanaji wa tuzo hiyo kwa NIC walifuata vigezo ikiwemo kufanya utafiti kwa nchi za Afrika Mashariki.
Amesema wameweza kuwafikia wananchi katika nchi hizo na kuwauliza kuhusu huduma za bima wanazotumia na kuona watu wengi wakivutiwa zàidi na huduma zinazotolewa na NIC.
“Ili kutoa hiki cheti cha Superbrand kwa taasisi na mashirika tunafanya utafiti wa kutosha ikiwemo utoaji wa huduma na ubora wa bidhaa kwa watumiaji katika sekta ya bima utafiti ulioonyesha watu wengi kuvutiwa na huduma zinazotolewa na shirika la bima la NIC” amesema Jaffer
Kampuni ya Superbrand imetoa tuzo kwa taasisi za umma na sekta binafsi Tano ambazo ni Shirika la bima la (NIC) NMB,Kampuni ya GSM.Kampuni ya bonite Bottles kupitia maji yake ya Kilimanjaro na Dar Caramica Center.